Breaking News

Your Ad Spot

Mar 10, 2011

MISS UTALII 2011 ATANGAZA VIPAUMBELE ATAKAVYOTEKELEZA KATIKA MUDA WAKE

ADELQUEEN Njozi, aliyejitwalia taji la Miss Utalii, katika fainali za shindano hilo, zilizofanyika hoteli ya Kiromo, Bagamoyo mkoa wa Pwani, Machi 3, mwaka huu, leo amezungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, na kueleza mikakati yake ya jinsi atakavyolitumikia taji hilo kwa faida ya taifa.
     Akizungumza katika ukumbi wa Idara ya Habari (MAELEZO), jijini, mrembo huyo(pichani) alisema,  kwanza ataanzisha kampeni kuhamasisha jamii kutumia sekta ya utalii kama nyenzo madhubuti ya kupambana na umasikini kwa kutumia vikundi vya ujasiriamali vya utalii.
     Mrembo huyo alisema katika hilo, vikundi hivyo vitafanya shughuli mbalimbali kama ususi, uchongaji, ufinyanzi na uchezaji ngoma, shonaji na uongozaji watalii.
      Alisema, jukumu lingine atakalobeba ni kuzunguka nchini kote kuhamasisha na kuelimisha jamii maana ya utalii, na faida zake kiuchumi kwa maendeleo ya taifa na kutumia taji lake kelimisha kina dada na vijana wanaojihusisha na biashara ya dawa za kulevya na ulevi wa kupindukia kuachana na mwenendo huo na badala yake wajihusishe na biashara ya utalii.
     Adelqueen alitoa mfano kwamba kinadada wanaojihusisha na biashara mbaya ya ukahaba, wanaweza kutumia uwezo wao na mvuto walio nao kushawishi watalii waje nchi kutembelea vivuto na hivyo kuwafaya wajipatie pato kubwa na halali.
      "Binafsi ninatumia taji langu kupiga vita uwindaji na uvuvi haramu na uharibifu wa mazingira na maliasili za taifa na kulitumia taji hili kuunga mkono juhudi za serikali katika kukuza utalii na utamaduni kwa kutafsiri kwa vitendo sera za taifa za utalii na utamaduni, huku nikitumia taji kuzitangaza, kuhamasisha jamii kutembelea hifadhi za taifa kutokana na kwamba hifadhi hizo ni moja ya vyanzo muhimu vya uchumi wa taifa", alisema.
      Alisema, atatumia fursa yake kutebea mashuleni na vyuoni kutoa elimu hiyo ya utalii na umuhimu wa utalii wa ndani huku akipiga vita mila na desturi za utamaduni potofu katika jamii, ikiwemo kukeketa, maujai ya vikongwe, albino kutokana na imani za kishirikiana, ubaguzi wa kisijinsia, ndoa za utotoni, urithishwaji wa wanawake baada ya waume zao kufariki.
    Aldelqueen aliahidi kushirikiana na warembo wenzake waliomfuatia, katika harakati zake, ili kuhakikisha Tanzania inaongeza pato la utalii duniani. Katika kinyang'anyiro kilichomuibua kuwa mshindi, wasichna 35 walichuana.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages