Breaking News

Your Ad Spot

Mar 10, 2011

TUZO KWA WAANDISHI BORA WA HABARI KUTOLEWA MLIMANI CITY MEI 3, MWAKA HUU

KAMATI ya maandalizi ya Tuzo za Umahiri wa waandishi wa Habari Tanzania (EJAT) imeandaa hafla ya
kuwazawadia waandishi wa habari waliojitutumua kwa umahiri mkubwa mwaka jana.


Akitangaza kuanza hafla hiyo, leo, mjini Dar es Salaam, Katibu Mtendaji wa Baraza la Habari Tanzania
MCT), Kajubi Mkajanga, alisema mshike mshike huo utakuwa Mei 3, mwaka huu, katika ukumbi wa Mlimani City, hapa hapa jijini.

Mkajanga alisema, Kamati ya Maandalizi ya sherehe hizo, inaongozwa MCT ikijumuisha Chama Cha
Waandishi wa Habari Wanawake Tanzania (TAMWA), Chama Cha Waandishi wa Habari za Michezo
(TASWA), HakiElimu, Chama Cha Waandishi wa Habari za Mazingira (JET), Jukwaa la Wahariri Tanzania
(TEF), Taasisi ya Uandishi wa Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN), Chuo Kikuu cha
Johns Hopkins na Chama cha Wamiliki wa Vyombo vya Habari Tanzania (MOAT).

Mukajanga amewaomba waandishi wa habari wanaotaka kushiriki kutuma kazi zao zilizochapwa gazetini au
kutanagazwa kwenye radio au televisheni kuanzia Januari 1, 2010 hadi Desemba 31, mwaka huu, na kwamba fomu za ushiriki zinapatikana MCT, kwenye tovuti ya MCT na zitasambazwa katika klabu za
waandishi wa habari na katika ofisi za vyombo vya habari.

Alisema, Kamati imeteua majaji watatu ambao alisema ni waadilifu, wanaoheshimika katika jamii na ambao
wana uzoefu katika masuala ya habari na vigezo vitazingatiwa vigezo maalum ambavyo vitatangazwa katika
vyombo vya habari vitafuatwa.


Mkajanga alisema, katika tuzo za mwaka huu, waandishi watashindanisha kazi zao katika makundi 16
aliyoyataja kuwa magazeti, radio na televisheni ni za Uandishi wa habari za Utawala Bora, Jinsia, uchumi na
biashara,Michezo na Burudani, Mazingira, Afya, Virusi vya Ukimwi na Ukimwi, Malaria, watoto, Elimu, Kazi na mahusiano kazini na Tuzo ya Mpigapicha bora.

Tuzo nyingine ni choraji bora wa vibonzo, habari za mawasiliano, Sayansi, teknolojia na habari za watu wenye ulemavu, huku kukiwa a kundi la wazi ambalo ni kwa ajili ya waandishi ambao kazi zao hazikuweza kuingia katika makundi hayo yaliyotajwa.

Alisema, Washindi wa kila kundi watazawadia vyeti, vikombe na zawadi ambazo zitatangazwa baadaye na
pia kutakuwa na mshindi wa jumla ambaye atafaidia kwa kufharamiwa masomo katika fani yoyote inayohusiana na habari ili mradi gharama hiyo isizidi dola 4,000 za Marekani
Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa kazini

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages