Breaking News

Your Ad Spot

Nov 22, 2013

CHADEMA WAMTUPIA VIRAGO ZITTO KABWE

Mh.Zitto Kabwe

MBUNGE maarufu wa Kigoma Kaskazini kupitia
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Zitto Kabwe, Mjumbe wa Kamati Kuu Dk. Kitila Mkumbo, na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha Samsoni Mwigamba wamevuliwa nyadhifa zao zote za uongozi na kubaki kuwa wanachama wa
kawaida. 

Aidha uongozi wa wabunge wa Chadema umeagizwa
na kamati kuu kumwandikia barua Zitto ya kumwondoa katika nafasi ya Naibu Msemaji wa Kambi ya Upinzani bungeni haraka iwezekanavyo kwa tuhuma za kukisaliti chama.

Uamuzi huo mgumu na mzito ulifikiwa juzi wakati wa Kikao cha Kamati Kuu (CC), kilichofanyika katika ukumbi wa Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.

Habari kutoka ndani ya kikao hicho kilichokuwa na mvutano mkubwa kwenye ajenda ya hali ya kisiasa ndani ya chama hicho, zilisema kuwa Zitto amevuliwa nyadhifa hizo baada ya kikao hicho kwa ajenda iliyoanza kujadiliwa tangu saa moja na nusu usiku na kumalizika saa kumi na nusu kisha kuwatia hatiani kwa makosa ya kukisaliti chama.

Akizungumza na Waandishi ofisi za chama hicho Makao Makuu, Mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe alisema “Chama ninachokiongoza ni cha watu, kinategemea maamuzi ya kikao, Katiba, Kanuni, maelekezo ya mabaraza ya Chama, miongozo ya shughuli za wabunge na viongozi wengine wenye nyadhifa katika Chama.”

Mbowe aliongeza kuwa kamati kuu ya chama hicho ni chombo cha kusimamia maadili ya chama, hivyo chama hakitakubali mtu yeyote, kwa sababu yake binafsi au ya kutumiwa kukiharibu chama.

Akisoma maazimio ya kamati kuu kuhusu tuhuma zinazomkabili Zitto Kabwe, Mwanasheria Mkuu wa Chama hicho Tundu Lissu alisema Uchunguzi wa Kamati Kuu umebaini kuwepo kwa mkakati mkubwa wa kutimiza malengo hayo ambao umeandikwa katika waraka unaoitwa ‘Mkakati wa Mabadiliko 2013.’ Mkakati huo uliandaliwa na kikundi kinachojiita ‘Mtandao wa Ushindi’ ambacho vinara wake wakuu ni wanne, yaani Naibu Katibu Mkuu na Naibu Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Mheshimiwa Zitto Zuberi Kabwe ambaye kwenye waraka huo anajulikana pia kama ‘MM’ au ‘Mhusika Mkuu’; mjumbe wa Kamati Kuu na mwanazuoni kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dk. Kitilla Mkumbo ambaye kwenye waraka anajulikana pia kama M1; 

Mwenyekiti wa Chadema Mkoa wa Arusha ambaye kwa sasa
amesimamishwa uongozi, Samson Mwigamba na ambaye kwenye waraka anaitwa M3; na mtu mwingine ambaye hadi sasa jina lake halijajulikana lakini kwenye waraka anajulikana kama M2 na anatajwa kuwa yuko ‘ukingoni kupigwa nje’ katika mageuzi ya kiutendaji yanayoendelea katika Sekretariat ya Chama hapa Makao Makuu.

Wakati hayo yakitokea, jana jioni, Makamu Mwenyekiti wa Chama hicho bara, na mbunge wa mpanda kati, Saidi Arfi alidaiwa kuandika waraka wa kujiuzulu nafasi hiyo kwa vigezo kuwa amekuwa akishutumiwa kwa kuchangia Waziri Mkuu Mizengo Pinda kupita bila kupingwa katika uchaguzi mkuu uliopita.

Waraka huo ambao haukuwa umesainiwa wala kuandikwa unaenda kwa nani, ulisomema “Napenda kuwasilisha kwako taarifa ya kujiuzulu nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara kuanzia Leo Ijumaa 22 Novemba 2013 kwa kuchoshwa na Unafiki unaoendelea
ndani ya Chama.

 Napenda ifahamike pia kwangu maslahi ya Wapiga kura, Wakaazi na wananchi wa Mpanda Mjini na Wilaya ya Mpanda ni muhimu katika kuwatumikia, hivyo basi sipo tayari kuchaguliwa marafiki. 

Kwa kipindi kirefu zimekuwepo shutma dhidi yangu na kutiliwa mashaka mahusiano yangu na Mhe Pinda Waziri Mkuu pamoja na kulijadili katika vikao kadha Mpanda na Dar es Salaam bado yapo mashaka kwa nini alipita bila kupingwa hayo yalikua maamuzi ya Wanampanda kwenu imekua ni tatizo lakin hamsemi kwa nini Majimbo mengine 16 nchini yalipita bila kupingwa mlikua wapi na nani alaaumiwe huu ni Unafiki  wa kupindukia.

Aidha mmechukizwa sana kwa nini nilihoji kauli ya Muasisi wa Chama Mhe. Mtei kutuchagulia viongozi naomba ifahamike wazi kwamba huu ni mtazamo wangu na utabakia hivyo siku zote kwa chama cha demokrasia kutoruhusu uongozi wa kiimla kwa kukidhi matakwa ya Waasisi ambao huvigeuza vyama kuwa.....

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages