Breaking News

Your Ad Spot

Aug 21, 2014

MOHAMED MATUMLA NA NASSIBU RAMADHANI KUZIDUNDA TENA SEPTEMBA 27 FRIENDS CORNER MANZESE


Bondia Mohamed Matumla kushoto na Nassibu Ramadhani wakitunishiana misuli.
 
Na Mwandishi Wetu
 MABONDIA Nassibu Ramadhani pamoja na Mohamed Matumla wameingia makubaliano ya kuzipiga kwa mara ya pili siku ya septemba 27 katika ukumbi wa Hoteli ya Friends Corner, Manzese, Dar es salaam

Akizungumzia mpambano huo mratibu wake Yassin Abdallah 'Ostadhi' amesema mabondia hawo wamekubaliana na kusaini mkataba wa kuzipiga siku hiyo ambapo mabondia hawo walikutana mara ya kwanza na bondia Mohamed Matumla alimshinda kwa point Nassibu Ramadhani hivyo kuufanya mchezo huu kuwa mgumu zaidi kwa Matumla kuendeleza kipigo au Ramadhani kurudisha kisasi katika mpambano huo siku hiyo kutakuwa na mapambano ya utangulizi

  Bondia Issa omari atamkabili juma fundi.kg 53 raundi nane. na Sadiq momba vs Tasha mjuaji kg 59 raundi nane. wakati Juma mustafa atamkabili Bakari dunda kg 61 raundi sita. huku kina dada Lulu  Kayage akipambana na fatma yazidu.kg 51 raundi nne.

siku hiyo pia kutakuwa na huuzwaji wa 
DVD ambazo zinatoa mwanga kwa mchezaji kujua mchezo na kufahamu zaidi mbinu mpya zitumiwazo na mataifa mbali mbali Duniani.

Wakiwemo mabondia bingwa wa dunia kama Manny Paquaio,Floyd Maywether,Amir Khani, Mohamed Ali ,Mike Tayson na wengine wengi wanaotamba na waliotamba katika mchezo huo wa masumbwi Duniani
 
kocha wa kimataifa wa mchezo wa masumbwi nchini Rajabu Mhamila 'Super D' ametoa wito kwa makampuni mbalimbali kujitokeza kutoa sapoti ya mchezo wa masumbwi kwani ndio mchezo pekee unaoweza kututoa kimasomaso watanzania tukafurahi HABARI/PICHA NA RAJABU MHAMILA

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages