Deogratias mongela/Ijumaa
MTOTO aitwaye
Badru Muhidin mwenye umri wa miaka miwili, amepata pigo kubwa baada ya
kukatwa uume wake kimakosa na babu yake aliyekuwa amempeleka kutahiriwa
kienyeji huko Mbagala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mama
mzazi wa mtoto huyo, Mwajuma Hussein ambaye ni mkazi wa Yombo jijini
Dar, alisema aliishi na mwanaye peke yake bila baba yake kwani
walitengana Juni mwaka jana baada ya kuishi bila kufunga ndoa kwa muda
mrefu, lakini mara kwa mara alikuwa akimpeleka mwanaye nyumbani kwa
wazazi wa mumewe kuwasalimia.
“Wiki
iliyopita babu yake Eliyasa alimuomba ili wakakae naye kwa muda mfupi,
baada ya muda mfupi walimtuma mtu akaniambia kuwa wameshamtahiri,
nilishangaa sana kwa kuwa hawakunitaarifu juu ya uamuzi huo, nikaenda
kumuona lakini wakawa wananikataza kumtazama sehemu za siri wakidai mila
zao haziruhusu kwa kipindi cha mwezi mzima.
“Kutokana
na shauku ya kutaka kuthibitisha hilo, siku hiyo nilipofika tu
nilimchukua na kumtazama hilo eneo ndipo nikabaini kuwa alikuwa amekatwa
katika kichwa, huenda huyo ngariba hakuwa mzoefu, kamfanyia kienyeji
lakini wengine wakisema huenda walitaka kufanya mambo ya kishirikina,”
alisema mama huyo.
Alisema
baada ya kumkuta katika hali hiyo, alianza kuhangaika naye hospitalini
kutafuta msaada, alipofika Temeke aliambiwa na madaktari.kwamba kijana
wake alikatwa vibaya na hivyo analazimika kufanyiwa upasuaji ili
kumnusuru.
“Madaktari
watatu walimuangalia na kwa kuogopa kumuathiri zaidi, waliniambia
niende Muhimbili, nimeumia sana, nahofia mwanangu akija kuwa mtu mzima
atakuwa goigoi tu, asije akawa shoga baada ya kukata tamaa kwa hali
iliyomtokea, japo wanasema kwa kuwa bado mdogo huenda ile sehemu ya
ngozi itaota lakini ndiyo maumbile yake yatakuwa na jeraha, hatokuwa
kama wanaume wengine.”
Babu
wa mtoto huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya kufunguliwa
shauri katika Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani kwa madai ya ukatili kwa
faili namba UKATILI WA MTOTO/MBL/RB/2251/2015 4/3/2015.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269