Breaking News

Your Ad Spot

Mar 13, 2015

IDADI YA WALIOFARIKI AJALI YA BASI NA LORI MAFINGA YAONGEZEKA



Idadi ya Vifo katika ajali iliyotokea jana mjini Mafinga Mkoani Iringa imeongezeka na kufikia watu 50 baada ya mtu mmoja kufariki dunia usiku wa kuamkia leo na miili mingine saba ambayo jana haikuhesabiwa, kugundulika mchana wa leo.


Kamanda wa Polisi mkoa wa Iringa Kamishna msaidizi wa Polisi Ramadahani Mungi amesema kuwa miili hiyo saba iliingizwa katika majokofu moja kwa moja kutoka katika eneo la ajali, hali iliyosababisha isihesabiwe huku akitaja majeruhi kuwa ni 22 na wawili kati yao wakiwa katika hali mbaya.


Shimo hili katikati ya barabara ndilo linasadikika kuwa chanzo cha ajali iliyoua watu 43 na zaidi ya 20 kujeruhiwa, katika eneo la Changarawe Mafinga Iringa.


Katika hatua nyingine Mwenyekiti wa chama cha NCCR Mageuzi James Mbatia ameitaka serikali kuchukua hatua kwa kila aliyehusika na kutokea kwa ajali hiyo, huku akitaka ufanyike uchunguzi wa kina ikiwa ni pamoja na kuchukua hatua za kutoruhusu malori kusafirisha mizigo katika barabara moja na mabasi ya abiria

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages