Breaking News

Your Ad Spot

Apr 15, 2015

PEMBA YAPIGA MARUFUKU UONESHAJI VIDEO USIOZINGATIA SHERIA

index
Na Masanja Mabula -Pemba .
Serikali ya Mkoa wa Kaskazini Pemba imepiga marufuku uoneshaji wa video usiozingatia sheria na taratibu katika sehemu za wazi ambazo zinamkusanyika wa watu .
Marufuku hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa huo Omar Khamis Othman baada ya kubaini kuwepo na watu wanaokiuka sheria makusudi na kuwataka kufuata taratibu zilizowekwa kwa mujibu wa sheria .
Akizungumza na masheha wa Wilaya ya Wete , Mkuu huyo wa Mkoa amesema kuwa mwananchi ambaye anataka kuonyesha video anapaswa kutaka kibali kutoka taasisi zinazohusika.
Aidha amewaagiza masheha kusimamia agizo hilo kwa kuhakikisha kwamba wanaoonyesha video wanakuwa na vibali halali kisheria .
"Nawaomba masheha mlisimamie agizo hili , hakikisheni kwamba wanaoonyesha video katika shehia zenu wanakuwa na vibali kutoka taasisi husika " aliagiza Mkuu wa Mkoa .
Ameeleza kwamba vitendo hivyo mbali na kutumika kisiasa , pia vimekuwa vikiwakosesha wanafunzi masomo yao kwani wanatumia muda wao mwingi kuangalia video hizo.
"Serikali ya Mkoa imebaini kwamba video hizo mbali na kutumika kisiasa lakini pia vimekuwa ni chanzo cha wanafunzi kukosa masomo yao kwani wanatumia muda wao mwingi kuangalia videoa badala ya masomo " alieleza .
Nao Masheha wameahidi kulisimamia agizo kwa kutoa elimu kwa wananchi kutambua athari za kuonyesha video bila ya kuwa na kibali kutoka taasisi husika .
Wamekiri kuwepo na wimbi la watu kuonyesha video hadharani bila ya kuwa na kibali na kwamba wameahidi kutoa elimu kwa wanaohusika na uoneshaji wa video .
"Kumekuwako na wimbi la uonyeshaji wa video katika shehia hasa nyakati za usiku , na wahusika hawana vibali ,kwa hili tutahakikisha kwamba tunatoa elimu kwa wananchi kutambua athari ya kuonyesha video kinyume na sharia " alieleza Sheha wa Shehia ya Utaani .
Uchunguzi uliofanywa na mwandishi wa habari hizi umebaini kwamba wanaoonyesha video kwenye mikusanyiko ya watu hasa nyakati za jioni na usiku hawana vibali jambo ambalo linaikosesha mapato serikali.(Muro)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages