Breaking News

Your Ad Spot

May 17, 2015

PAPA FRANCIS KUTAWAZA WATAWA 2 WAPALESTINA


Papa Francis kutawaza watawa 2 wapalestina

Makabiliano baina ya Israeli na Wapalestina yamesababisha wakritu kupungua mashariki ya kati.

Kiongozi huyo wa kanisa katoliki alimtunuku Abbas medali ya Amani huku akimtaja kuwa ''malaika wa amani''
Kiongozi wa kanisa Katoliki duniani Papa Francis atawatawaza watawa wawili wa Kipalestina walioishi katika karne ya 19 wakati wa utawala wa Ottoman.
Watawa hao waili walioishi miongoni mwa jamii ya wapalestina waarabu ,bi Marie Alphonsine Ghattas na Mariam Bawardy watakuwa miongoni mwa watakatifu watakao tawazwa hii leo katika ukumbi wa kanisa kubwa la papa Francis la St Peter's Square iliyoko Rome.
Rais wa Palestina Mahmoud Abbas ni miongoni mwa mahujaji 2,000 wakristo waliofika katika makao makuu ya kanisa katoliki huko Vatican.
Hatua hii inatazamwa na wengi kama chambo cha kuwavutia wakristu katika maeneo ya mashariki ya kati ambapo wakristu wanahujumiwa na jamii.
Aidha wengi wanashuku kuwa Vatican imetamausha na idadi ndogo ya wakristu katika eneo iliyochipukia miaka elfu mbili iliyopita.
Hapo jana Papa Francis alifanya mazungumzo na rais wa wapalestina Mahmoud Abbas katika makao makuu ya Vatican.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki alimtunuku Abbas medali ya Amani huku akimtaja kuwa ''malaika wa amani''
Ziara ya Bwana Abbas imewadia siku chache tu tangu makao makuu ya kanisa katoliki duniani kutambua rasmi taifa la Kipalestina.
Watawa hao Marie Alphonsine Ghattas - aliyezaliwa katika familia ya kipalestina mjini Jerusalem alianzisha huduma ya watawa ya - Rosary Sisters, ambayo hadi wa leo inaendesha shule za chekechea na zile za msingi.
Kwa upande wa wake bi Mariam Bawardy alizaliwa Galilaya katika familia moja yenye asili ya Syria na Lebanon japo alikuwa akihudumu katika kanisa katoliki la Ugiriki .
Bi Mariam anasemekana kuwa alitenda miujiza miongoni mwa jamii yake huku akitambuliwa kwa kuonekana na alama za ishara ya kusulubishwa kwa Yesu Kristo msalabani.
Wawili hao waliishi katika enzi ya Ottoman ambapo wanawake hawakuwa na semi katika hali halisi ya maisha lakini waliibuka kuwa mifano ya kuigwa licha ya kuishi maisha ya uchochole na magonjwa mengi.
Wawili hao vilevile wanadaiwa kuwa na mawasiliano na mamake Yesu Kristo Maria Mtakatifu.
Kutawazwa kwao kunatarajiwa kuweka msingi yao kutambuliwa kama watakatifu kutoka kwenye chimbuko la ukristu.
takwimu zinaonesha kuwa idadi ya wakristo imedidimia kwa asili mia 2% katika eneo la Palestina na Israili.
Hii inatokana na umaarufu mkubwa wa Waislamu na Wayahudi ambao kwa kiasi kikubwa wamekuwa wapigana na kuwalazimu wakristu kutorokea mataifa salama kuepuka vita

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages