Mkurugenzi
Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa Ubongo na
Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (kushoto) akizungumza na
wandishi wa Habari (pichani hawapo) baada ya hitimisho la Mkutano wa
nne wamafunzo ya Upasuaji wa Ubongo , uti wa mgongo na mishipa ya
fahamu, Mkutano huo ulifunguliwa na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii
Dkt Seif Rashid, uliomalizika hivi karibuhuo na wali walifanya
upasuaji wakishirikiana na Wataalamu madaktari bingwa wa Chuo cha
Weill Cornell toka Marekani kufanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia
mashine ya kisasa ambapo Watanzania 21 wamefanyiwa upasuaji wa
magonjwa hayo wakishirikiana na madaktari toka Tanzania , Uganda,
Rwanda, Southi Afrika, Marekani na Ulaya. Dokta Othman Kiloloma,
alimshukuru Rais Jakaya Kikwete ambaye aliye waweka karibu na wenzao wa
Chuo cha Marekani na kuwashukuru wenzao wa chuo cha marekani kwa
kuwawezesha kufanyika upasuaji huo (wakwanza kulia) ni Mkuu wa
Idara ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu
Dk.Hamisi Shabani,amye aliwaeleza waandishi hao kua mgonjwa mmoja
kufanyiwa upasuaji anagharimu kiasi cha dola elfu moja za upasuaji huo
nahaihusiani na mambo mengine mbali na katikati ni Profesa Philip Steg
toka Chuo cha Marekani nayeye alipata nafasi ya kuongea na waandishi hao
na kuwashukuru Wataalamu wa Moi (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa,ajali na upasuaji wa
Ubongo na Mishipa ya Fahamu (MOI) Dokta Othman Kiloloma (wapili) kushoto na kuanzia kulia ni Mkuu wa Idara ya upasuaji wa ubongo, uti wa mgongo na mishipa ya fahamu Dk.Hamisi Shabani anaye fatia ni Profesa Philip Steg toka Chuo cha Weill Cornell Marekani na kushoto ni Meneja ea Taasisi ya Moi Almas Jumaa.
Madaktari wakiwakatika Upasuaji na ikiongozwa Dk, Japhet Ngerageza
Mashine
ya kisasa yenye thamani shilingi mil. 700 iliyotolewa msaada na Weill
Cornell toka Marekani ikikumika kusaidia kuokoa maisha ya Watanzania kwa
Muungano wa jitihada za Rais Jakaya Kikwete
Madaktari
Bingwa wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa ya Fahamu
(MOI) wakishirikiana na madaktari bingwa wa Chuo cha Weill Cornell toka
Marekani kufanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia mashine ya kisasa ambapo
wagonjwa 21 wamefanyiwa upasuaji wa magonjwa hayo. Dar es Salaam
Madaktari Bingwa wa Taasisi ya Mifupa na Upasuaji wa Ubongo na Mishipa
ya Fahamu (MOI) wakishirikiana na madaktari bingwa wa Chuo cha Weill
Cornell toka Marekani wakionyeshana jambo wakati walipokuwa wafanya upasuaji wa mgongo kwa kutumia mashine ya
kisasa ambapo wagonjwa 21 wamefanyiwa upasuaji wa magonjwa hayo. Dar
es Salaam
Madaktari wakiwa katika chumba cha Upasuaji
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269