Ushahidi
wa upande wa Utetezi wa mshtakiwa wa pili, Waziri wa zamani wa Nishati
na Madini, Daniel Yona kuendelea kusikilizwa leo na Mahakama ya
Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya jana mwenyekiti wa jopo la mahakimu
wanaosikiliza kesi hiyo, Jaji John Utamwa kuwa na udhudu wa kikazi.
Jaji
Utamwa na Jaji Samu Rumanyika walianza kusikiliza kesi hiyo wakiwa
Mahakimu Wakazi Wakuu kabla ya kupanda na kuwa Majaji wa Mahakama Kuu
Tanzania, ambao kwa sasa wako, Kanda ya Tabora.
Kesi hiyo iliahirishwa jana na jopo la mahakimu wawili Rumanyika na Hakimu Mkazi Mkuu, Saul Kinemela.
Pande zote mbili ziliridhia sababu hiyo na kesi hiyo itaendelea kusikilizwa utetezi wa Mshtakiwa wa pili Yona, hapo leo.
Washtakiwa
wengine ni, Waziri wa zamani wa Fedha, Basil Mramba na Katibu Mkuu wa
zamani wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja wote wanakabiliwa na kosa la
matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia Serikali hasara ya Sh.
bilioni 11.7 kwa kutoa msamaha wa kodi kwa Kampuni tanzu ya Alex Stewart
( ASSAYERS) Government Business Corporation.
Katika
kesi ya msingi, washtakiwa wanadaiwa kuwa, kati ya Agosti mwaka 2002 na
Juni 14 mwaka 2004 jijini Dar es Salaam, wakiwa watumishi wa umma kama
mawaziri na katibu mkuu walitumia vibaya madaraka.
Ilidaiwa
kuwa kwa kupitia kampuni ya Alex Stewart (ASSAYERS) ya Uingereza
iliyoingia mkataba wa ukaguzi wa madini ambapo kwa kupitia kampuni tanzu
ya Alex Stewart ( ASSAYERS) Government Business Corporation waliingia
mkataba kukagua kiwango cha uzalishaji wa madini ya dhahabu kinyume cha
Sheria ya Manunuzi ya Umma.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269