Aliyewahi
kuwa waziri mkuu wa Uingereza kuanzia mwaka 1940 hadi 1945 na kisha
kurejea tena mwaka 1951 hadi 1955, Winston Churchill aliwahi kusema, “a
pessimist sees the difficulty in every opportunity; an optimist sees the
opportunity in every difficulty.”
Alimaanisha kuwa “mtu muoga huona ugumu kwenye kila fursa na mtu jasiri huona fursa kwenye kila ugumu.”
2014 ulikuwa ni mwaka wenye majaribu na mitihani mingi kwa Sitti Mtemvu.Mara
tu baada ya kushinda taji la Miss Tanzania 2014, skendo moja baada ya
nyingine zikaanza kuibuka. Kubwa lilikuwa ni kitendo chake cha kudaiwa
kudanganya umri na kuwasilisha cheti cha kuzaliwa ‘feki.’
Pia watu wakazusha kuwa mrembo huyo ana mtoto, kitu ambacho ni kinyume cha vigezo vya shindano hilo lililofungiwa mwaka jana.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269