Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Missenyi mkoani Kagera ikiwa muendelezo wa ziara za kujenga na kuimarisha chama, kukagua,kuhimiza na kusimamia utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM.
Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM wilaya ya Missenyi wakifurahia jambo wakati wa hotuba ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana ambaye anafanya ziara nchi nzima ya kujenga na kuimarisha chama.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akiteremka kwenda kuona chanzo cha maji kwenye eneo la Ukolobe kijiji cha Rukurungo kata ya Bugandika wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.
Watoto wakichezea maji karibu na chanzo cha maji katika kijiji cha kijiji cha Rukurungo kata ya Bugandika wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipandisha kilima kutoka kukagua tanki la maji katika mradi wa maji katika kijiji cha Rukurungo kata ya Bugandika wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndugu Nape Nnauye akisalimia wakazi wa kijiji cha kijiji cha Rukurungo kata ya Bugandika wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akinywa maji wakati wa uzinduzi wa huduma ya maji itakayohutumia wakazi zaidi ya 1884 na itakua na vituoa zaidi ya 16 katika kijiji cha Rukurungo kata ya Bugandika wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Mhe. Assumpta Mshama akihutubia wakazi wa kata ya Bwanjai.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Bwanjai ikiwa sehemu ya ziara ya Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana katika wilaya ya Missenye mkoani Kagera.
Balozi Dk. Diodorus Kamala akiwasalimia wakazi wa kata ya Bwanjai waliojitokeza kwa wingi kuja kumpokea na kumsikiliza Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana.
Mbunge wa Jimbo la Nkenge Mhe. Assumpta Mshama (kulia) akiongea na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye pamoja na Balozi Balozi Dk. Diodorus Kamala kwenye eneo la mkutano katika kata ya Bwanjai.
Wananchi wakiwa kwenye mkutano wa hadhara nje ya ofisi ya kata ya CCM Bwanjai.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Bwanjai mbele ya ofisi ya Kata ya CCM .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akipiga ngoma aliyopewa na Wazee wa Kimila wa Kata ya Bwanjai.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Mzee Omari Hussein ambaye ni mmoja wa Walezi waliomlea wakati wa ujana wake.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa kukagua ujenzi wa shule ya Kiislam katika kata ya Kyaka
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa kata ya Mtukula,wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa Mtukula ,mkoani Kagera.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akihutubia wakazi wa Bunazi kwenye uwanja wa Bunazi maarufu kama uwanja ambao wanajeshi walijipongeza baada ya kumaliza vita .
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa kata ya Bunazi ambapo aliishauri serikali kupunguza vikwazo kwa wafanya biashara wa mipakani.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akisisitiza jambo kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika wilaya ya Missenyi mkoani Kagera.
(Picha zote na Adam Mzee)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269