A
Mgombea
mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia
Suluhu (katikati) akimnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Mbinga Vijijini,
Martin Mtonda (kushoto) na mgombea udiwani wa CCM.
MGOMBEA
mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia
Suluhu ameanza ziara yake mkoani Ruvuma akiinadi ilani ya chama hicho
huku akiahidi neema kwa wakulima wa kahawa na mahindi wa mkoa huo.
Bi. Samia
Suluhu ambaye amehutubia mikutano mitatu katika majimbo mawili ya mkoa
wa Ruvuma yaani Jimbo la Nyasa na Mbiga Vijijini, akizungumza katika
mikutano yake amesema serikali itakayoundwa na CCM endapo itashinda
itahakikisha inashusha umeme katika vijiji vyote vya mkoa huo kwa awamu
ili kuchochea maendeleo ya wananchi.
Alisema
kwa kuwa mkoa huo unazalisha mazao ya mahindi na kahawa serikali
itahakikisha inaanzisha viwanda eneo hilo vya kusaga na kuandaa unga wa
mahindi kwa wakulima na kuwawezesha ili wauze unga na kunufaika zaidi
tofauti na ilivyo kwa sasa ambapo wamekuwa wakilanguliwa.
Alisema
viwanda vingine ambavyo Serikali ya CCM itavianzisha ni pamoja na
viwanda vya kubangua kahawa na kuiandaa kikamilifu tayari kwa kutumika,
jambo ambalo alisema licha ya kuongeza thamani ya zao hilo itaongeza
ajira kwa vijana na kuchochea uchumi wa wakulima eneo hilo.
Akizungumzia
miundombinu ya barabara ambayo bado ni changamoto kwa mkoa huo hasa
vijijini alisema serikali itakayoundwa na CCM chini ya uongozi wa Dk.
John Pombe Magufuli pamoja na yeye watahakikisha wanajenga na kuboresha
barabara za maeneo hayo ili ziweze kupitika kwa uhakika.
Hata
hivyo kiongozi huyo amesema Serikali itakayoundwa na CCM endapo
itashinda Uchaguzi Mkuu wa Oktoba, 2015 imejipanga kuboresha vizuri
huduma za afya kuondoa ukiritimba na rushwa, elimu kwa kutoa elimu bure
toka darasa la kwanza hadi kidato cha nne pamoja na ujenzi wa mabweni na
uwezeshaji vijana na akinamama kiuchumi popote walipo mjini na
vijijini.
Ziara ya
mikutano ya kampeni ya mgombea mwenza huyo wa urais tiketi ya CCM,
inaendelea leo katika Mkoa wa Ruvuma na ataingia Jimbo la Tunduru
kuendelea kuinadi ilaya ya chama hicho kuomba ridhaa kwa wananchi ili
waweze kurejeshwa madarakani na kuunda dola.
Pichani
juu ni baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamefurika katika kiwanja
cha Kijiji cha Maguu Wilaya ya Mbinga kumsikiliza mgombea mwenza wa
urais kupitia tiketi ya CCM alipokuwa akiinadi ilani ya chama hicho.
Pichani
juu ni baadhi ya wananchi na wanaCCM wakiwa wamefurika katika kiwanja
cha Kijiji cha Maguu Wilaya ya Mbinga kumsikiliza mgombea mwenza wa
urais kupitia tiketi ya CCM alipokuwa akiinadi ilani ya chama hicho.
Baadhi ya wananchi na wanaCCM wa Kijiji cha Maguu wilayani Mbinga wakimsubiri mgombea mwenza wa urais, CCM, Bi. Samia Suluhu.
Pichani
juu ni baadhi ya pikipiki maarufu kwa jina la bodaboda zilizompokea
mgombea mwenza wa CCM urais, Bi. Samia Suluhu mara baada ya kuingia
Wilaya ya Mbinga zikiwa zimeegeshwa pembeni huku mkutano wa hadhara
ukiendelea.
Mmoja wa
wajumbe wa kamati ya kampeni ya mgombea mwenza, Bi. Asumpta Mshama
akizungumza na wanaCCM na wananchi (hawapo pichani) katika Kijiji cha
Maguu, Wilaya ya Mbinga.
Mgombea
mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia
Suluhu (kulia) akizungumza na Mjumbe wa Kamati ya Siasa Mkoa wa Ruvuma,
Said Mwambungu, kabla ya kuanza kuhutubia katika mikutano wake wa
kampeni.
Mgombea
mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia
Suluhu (katikati) akizungumza na baadhi ya viongozi wa CCM ambao ni
wenyeji wake mkoa wa Ruvuma.
Mgombea
mwenza wa nafasi ya urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM), Bi. Samia
Suluhu (katikati) akizungumza na mmoja wa vijana walemavu waliohudhuria
mkutano wake wa hadhara Kijiji cha Maguu. Bi. Suluhu alimsaidia fedha
kijana huyo.
*Imeandaliwa na www.thehabari.com
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269