Mgombea
Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa tiketi ya chama cha
Mapinduzi (CCM),Dkt John Pombe Magufuli akifafanua jambo mbele ya maelfu
ya wakazi wa jiji la Tanga waliojitokeza kwenye mkutano wa hadhara wa
kampeni,uliofanyika katika viwanja vya Tangamano jioni ya leo mjini
Tanga.
Mgombea
wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji
wa Tanga kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika katika viwanja vya
angamano,jioni ya leo ambapo aliahidi kuboresha Bandari ya Tanga,
kujenga Viwanda vya matunda na samaki ili kuweza kupunguza tatizo kubwa
la ajira kwa vijana.
Wakazi wa mji wa Tanga waliofika kwenye mkutano huo wakishangilia jambo.
Nyomi la watu .
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli akisalimiana na Naibu Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mheshimiwa Mwigulu Nchemba
Naibu
Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni mgombea
Ubunge wa Jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba akihutubia wakazi wa mji
wa Tanga kwenye mkutano wa kampeni za CCM.
Sehemu
ya umati wa wakazi wa mji wa Tanga na vitongoji vyake wakiwa wamefurika
kwenye viwanja vya Tangamano kwenye mkutano wa kampeni za CCM,ambapo
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli aliwahutubia wananchi hao.
Dkt
Magufuli akisisitiza jambo mbele ya maelfu ya wananchi (hawapo pichani)
jioni ya leo kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika uwanja wa
Tangamano.
Naibu
Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akihutubia wakazi wa Tanga mjini kwenye
mkutano uliofanyika kwenye uwanja wa Tangamano.
Naibu Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia ambaye pia ni mgombea Ubunge wa Jimbo la Bumbuli Mhe. January Makamba na Naibu
Waziri wa Fedha na mgombea ubunge wa Jimbo la Iramba Magharibi
Mheshimiwa Mwigulu Nchemba wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri kwenye
mkutano wa kampeni jioni ya leo katika uwanja wa Tangamano,ambapo
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli alihutubia na Kumwaga sera zake kwa
wananchi,ikiweno na kuomba ridhaa ya kuwaongoza katika miaka mitano
ijayo.
Katibu
Mkuu Mstaafu wa CCM Mzee Yusuph Makamba akihutubia wakazi wa Tanga
mjini kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika ndani ya viwanja vya
Tangamano.
Maelfu
ya Wananchi wakimsikiliza Dkt Magufuli alipokuwa akimwaga sera zake na
kuwaomba wananchi hao wajitokeze kwa wingi Oktoba 25 na kumpigia kura ya
ndio ili aibuke mshindi na kupewa ridhaa ya kuiongoza Tanzania katika
awamu ya tano.
Mgombea
Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwaaga wananchi wa mji wa Tanga
waliofika kwenye mkutano hadhara wa kampeni,uliofanyika jioni ya leo
katika viwanja vya Tangamano mjini humo na kuhudhuriwa na umati mkubwa
wa watu.
PICHA NA MICHUZI JR-TANGA
PICHA NA MICHUZI JR-TANGA
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269