Jina
la mchezaji Wayne Mark Rooney limekua gumzo nchini England wiki hii
hasa pale ambapo alikua amebakiza goli moja tu kuwa mfungaji bora wa
muda wote wa timu ya taifa ya England, akimpita Sir Bob Charlton
aliyeshikilia rekodi hiyo kwa kipindi cha miaka 45.
Wazza
alifunga goli hilo la rekodi la 50 katika timu ya taifa na kumfanya
sasa kuwa ni legendari wa England, heshima aliyoipata baada ya muda
mrefu sana tangu akiwa na miaka 17 alipoibuka katika timu ya taifa.
Baada
ya kufunga goli hilo la 50 dhidi ya Switzerland, mashabiki waliofurika
katika uwanja wa Wembley waliripuka na kuimba, “Rooney! Rooney! Rooney!”
huku Rooney mwenyewe akijikuta mwenye hisia kubwa baada ya kuweka
historia hiyo.
Wachezaji
mbalimbali wa zamani na sasa, kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii
wameandika kumpongeza nahodha huyo mwenye miaka 29 kwa kuandika
historia hiyo katika maisha yake ya soka.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269