Baada
ya kuvunja rekodi na kuwa mfungaji bora wa timu ya taifa ya England kwa
kufikisha magoli 50 hivi sasa, Wayne Rooney alijikuta mwenye hisia
kubwa mbele ya wachezaji wenzake na mashabiki waliokuwa wakimpongeza
mara baada ya kufunga kwa mkwaju wa penati katika dakika ya 84.Rooney
mwenye miaka 29 alitokwa na machozi huku akinyoosha mikono juu ishara
ya kumshukuru Mungu kwa mafanikio aliyoyapata katika maisha yake ya
soka.
Akiongea
katika chumba cha kubadilishia nguo baada ya kuombwa kufanya hivyo na
kocha Roy Hodgson, Wayne amesema ni wakati mkubwa na muhimu kwake na
familia yake huku akiwapa changamoto vijana Raheem Sterling, Harry Kane
na Ross Barkley kukomaa na kufikia hadi kupita rekodi yake siku zijazo.
Wachezaji
lukuki wakiongozwa na David Beckham wamempongeza mchezaji huyo huku
nahodha wa Chelsea, John Terry akienda mbali zaidi kwa kusema Rooney
ndiye mchezaji bora zaidi kuwahi kuzaliwa England.
Chama
cha soka England, FA kitamfanyia sherehe nahodha huyo wa England mwezi
ujao katika mechi ya kufuzu itayofanyika Wembley katika usiku utakaoitwa
Wayne Rooney ambapo atakabidhiwa kiatu cha dhahabu na Sir Bob Charlton
ambaye ndiye alikua akishikilia rekodi hiyo kwa miaka 45 sasa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269