Ndege ya British Airways ikiungua katika Uwanja wa Ndege wa McCarran uliopo Las Vegas.
Ndege ya British Airways aina ya Boeing 777 baada ya kuzimwa moto huo.
Abiria wakishuka katika ndege hiyo baada ya moto kuzimwa.
Ndege hiyo baada ya kuzimwa moto.
Picha iliyopigwa na abiria aliyekuwa kwenye ndege nyingine.
NDEGE ya
British Airways iliyokuwa na watu 172 imeungua wakati ikijiandaa kupaa
kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa McCarran uliopo Las Vegas nchini
Marekani jana usiku.
Katika ajali hiyo, watu 14 wamejeruhiwa na kupelekwa hospitali kwa matibabu ila hakuna mtu aliyepoteza maisha.
Ndege hiyo
aina ya Boeing 777 ilikuwa inajiaanda kupaa kuelekea jijini London
wakati ilipoanza kuwaka moto baada ya kupata hitilafu katika mfumo wake
wa injini.
Vikosi vya zimamoto katika Uwanja wa McCarran vilifanya kazi ya ziada kuzima moto huo kabla ya kuleta madhara makubwa.
Majeruhi katika ajali hiyo wengi walipata madhara kutokana na moshi mkubwa uliokuwa ukitoka katika ndege hiyo.
Kati ya watu waliokuwa kwenye ndege hiyo, 159 walikuwa abiria huku 13 wakiwa wafanyakazi wa ndege hiyo.
Credit: Daily Mail
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269