Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk.Binilith Mahenge (kulia), akikata
utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha oparesheni cha Kampuni ya
MagilaTech, iliyotengeneza teknolojia ya tigo backup inayowezesha
kurejesha kumbukumbu na kuzuia wizi wa simu za mkononi Dar es Salaam
leo.
Wanahabari na wadau wengine wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo.
Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez (kulia), akitoa hutuba yake.
Mkurugenzi
Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech), Dk. Hassan
Mshinda (kulia), akizungumza katika uzinduzi huo. Kushoto ni Mwenyekiti wa Bodi ya DBTi, Balozi Ami Mpungwe.
Waziri
Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk.Binilith Mahenge, kwa niaba ya
Makamu wa Rais Dk.Mohammed Gharib Bilal aliyekuwa mgeni rasmi katika
uzinduzi huo akisoma hutuba.
Meneja
wa mradi huo kutoka Tigo, Atuletye Mwamila (kulia), akielekeza jinsi
teknolojia hiyo inavyofanya kazi na kuwezesha kuipata simu iliyopotea na
kumbukumbu.
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magila Tech iliyotengeneza Teknolojia ya Tigo Backup, Godfrey Magila akielezea jinsi teknolojia hiyo inavyofanya kazi.
Mwenyekiti
wa Bodi ya DBTi, Balozi Ami Mpungwe (kushoto), akizungumza katika
uzinduzi huo. Kulia ni Mkurugenzi Mkuu wa Tume ya Taifa ya Sayansi na
Teknolojia (Costech), Dk. Hassan Mshinda.
Wanahabari wakiwa kwenye uzinduzi huo.
Maofisa
wa ufundi, Rahim Hussen (kushoto) na Mkupete Mkamba (kulia), wakitoa
maelezo wa kifaa mfano wa ndege kinachorushwa angani na kuweza kubaini
magonjwa katika mimea walicho kibuni.
Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Binilith Mahenge (katikati),
akikata utepe kuashiria uzinduzi wa kituo cha oparesheni cha Kampuni
ya Magila Tech, iliyotengeneza teknolojia ya tigo backup inayowezesha
kurejesha kumbukumbu na kuzuia wizi wa simu za mkononi Dar es Salaam
leo, kilichopo Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (Costech). Kituo
hicho kinashirikiana na kampuni ya simu ya tigo, Dar Teknohama Business
Incubator (DTBi), pamoja na Costech kuendesha mradi huo. Kutoka kulia ni
Meneja Mkuu wa Tigo, Diego Gutierrez, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Magila Tech iliyotengeneza Teknolojia ya Tigo Backup, Godfrey Magila na Ofisa Mtendaji Mkuu wa DTBi, Mhandisi George Mulamula
Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Magila Tech iliyotengeneza Teknolojia ya Tigo
Backup, Godfrey Magila (kulia), akitoa maelezo kwa Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk. Binilith Mahenge jinsi kituo hicho cha oparesheni kinavyofanya kazi.
Na Dotto Mwaibale
KAMPUNI ya
Mawasiliano ya simu ya Tigo kwa kushirikiana na Kituo cha Kukuza Vijana
Wenye Mawazo ya Sayansi na Teknolojia (DTBi), wamezindua huduma
itakayowawezesha watumiaji wa simu za kisasa (smartphone) kurejesha
kumbukumbu na kupatikana kwa simu iliyopotea au kuibiwa.
Akizungumza
kabla ya kuzinduliwa rasmi huduma hiyo Makao Makuu ya Tume ya Taifa ya
Sayansi na Teknolojia (Costech), Dar es Salaam leo asubuhi, Waziri wa
Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Dk.Binilith Mahenge, Meneja Mkuu
wa Tigo, Diego Gutierrez, alisema huduma hiyo inaitwa 'Tigo Backup'
itakuwa na uwezo wa kurudisha majina yote kwenye simu, picha, video,
ujumbe mfupi 'sms' na vitu vingine vilivyopotea.
Alisema
mteja ataweza kugundua na kurejesha simu zao zilizopotea au kuibiwa na
pia huduma hiyo itamuwezesha mteja kuwa na uwezo wa kupata picha ya
aliyemuibia kwani simu itapiga king'ora.
"
King'ora hicho kitaonesha simu ilipo, simu itajifunga ili kuzuia
matumizi mabaya, kumjulisha mwenye simu pindi abadilishapo laini na
kwamba huduma hiyo imebuniwa na mwanafunzi mzawa kutoka DTBi ," alisema
Gutierrez.
Kwa
upande wa Waziri, Dk. Mahenge alizishukuru kampuni hizo kuwajengea
uwezo na kuwawezesha Watanzania kuleta maendelea katika nchi yao na
kujijengea utajiri kupitia ubunifu huo.
Alisema
Tanzania nchi inayoungwanishwa kidigitali zaidi kwa kutumia sismu
kuliko kompyuta na kwa mujibu wa takwimu za watumiaji wa simu zinaonesha
kuna ongezeko kubwa kutoka watu milioni 2.96 mwaka 2005 hadi milioni 33
mwaka huu.
Alisema
kwa kutambua nchi ni changa ambayo watu wake asilimia 50 ni vijana,
wamejikita katika kutoa elimu ya ufundi katika sayansi na teknolojia
yenye ubunifu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269