Breaking News

Your Ad Spot

Sep 11, 2015

RAIS KIKWETE AAGANA NA WAFANYAKAZI WA MAHAKAMA YA AFRIKA

10
Rais wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu Jaji Agustino Ramadhani akimkaribisha Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete katika uwanja wa ndege wa Arusha ambapo alikutana na kuagana na majaji na watumishi wa Mahakama ya Afrika mjini Arusha leo.
11

9
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akisaini kitabu cha wageni katika ofisi ya Rais wa Mahakama ya Afrika na Haki za Binadamu iliyopo mjini Aruha huku Rais wa Mahakama hiyo Jaji Agustino Ramadhani kulia akishuhudia.
1
2
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete na Rais Wa Mahakama ya Afrika ya Haki za binadamu Jaji Agustino Ramadhani wakizindua kitabu cha taarifa za msingi kuhusu mahakama hiyo kwenye Ukumbi wa Kibo kwenye majengo ya Mahakama hiyo mjini Arusha leo.Rais Kikwete alitumia fursa hiyo kuagana na viongozi na wafanyakazi wa mahakama hiyo.
35
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwahutubia wafanyakazi na viongozi wa Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu mjini Arusha leo.
78  
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na viongozi na wafanyakazi wa Mahakama ya aFrika ya Haki za binadamu mjini Arusha wakati Rais alipotoa hotuba ya kuwaaga.
(Picha na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages