Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum (wa tatu
kushoto) na wenzake wakichezea mpira kujaribu viwango vya mipira hiyo
baada ya kukabidhiwa na Kamanda wa kanda maalumu ya Dar es Salaam,
suleiman Kova (wa pili kulia), wakati wa mazoezi ya timu ya Kamati ya
Amani inayoundwa na Viongozi wa Dini. Mazoezi hayo yalifanyika leo
asubuhi kwenye Uwanja wa Karume jijini Dar es Salaam, sambamba na timu
ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zaoTanzania,kwa ajili ya maandalizi ya
mchezo wakirafiki kati yao unaotarajia kuchezwa hivi karibuni.
Kamanda
wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova (kulia) akimkabidhi
mpira Nahodha wa timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini, Skei Mkuu
wa Mkoa wa Dar es Salaam,Sheikh Alhad Mussa Salum, baada ya mazoezi ya
timu hiyo na timu ya Mabalozi wanaoziwakilisha nchi zao Nchini,
yaliyofanyika kwenye Uwanja wa Karume jijini leo asubuhi kwa ajili ya
maandalizi ya mchezo wa kirafiki unaotarajia kuchezwa hivi karibuni.
Mazoezi ya pamoja…
Suleiman Kova, akisalimiana na Mabalozi baada ya kuwakabidhi mipira leo asubuhi.
Picha
ya pamoja ya Timu ya Kamati ya Amani ya Viongozi wa Dini na Mabalozi
baada ya mazoezi yao ya pamoja yaliyopigwa kwenye Uwanja wa Karume
jijini Dar leo asubuhi.
Sheikh
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Sheikh Alhad Mussa Salum, akijaribu
kumpiga chenga Balozi wa Denimark, wakati wa mazoezi yao ya pamoja
kwenye Uwanja wa Karume Dar es Salaam leo asubuhi kwa ajili ya kujiandaa
na mchezo wa kirafiki.
Mazoezi ya Viungo…..
Nahodha akizungumza na wachezaji wake baada ya mazoezi
Majadiliano baada ya mazoezi…Picha na www.sufianimafoto.com
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269