Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando (kulia),
akibonyeza kitufe kuashiria uzinduzi wa mfumo wa taarifa ya vituo vya
afya nchini uliofanyika Dar es Salaam leo asubuhi. Kushoto ni Mkuu wa
Kitengo cha Tehama wa wizara hiyo, Hermes Rulagirwa na Ofisa wa
Tehama, Kenani Mwansasu.
Hapa ni kupongezana baada ya uzinduzi huo.
Mkuu wa Kitengo cha Tehama wa wizara hiyo, Hermes Rulagirwa (kulia), akizungumza na wanahabari.
Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wakiwa kwenye uzinduzi huo uliofanyika Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Jengo la Ubungo Plaza.
Wadau mbalimbali wa sekta ya Afya wakiwa kwenye uzinduzi huo uliofanyika Hoteli ya Blue Pearl iliyopo Jengo la Ubungo Plaza.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Mgeni rasmi katika uzinduzi huo Katibu
Mkuu Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk.Donan Mmbando (katikati),
akiwa katika picha ya pamoja na wadau wa sekta ya afya wakati wa
uzinduzi huo.
Na Dotto Mwaibale
SERIKALI
imezindua mfumo mpya wa kuhifadhi taarifa za vituo vya huduma ya afya
vya Serikali na binafsi katika ngazi ya kanda, mtaaa kijiji na mkoa
nchini.
Akizungumza
Dar es Salaam leo asubuhi wakati akizindua mfumo huo , Katibu Mkuu wa
Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Donan Mmbando alisema kupitia
mfumo huo watumiaji watapata taarifa za vituo sahihi na namna vinavyotoa
huduma.
Alisema
mfumo huo utatumik kama chanzo pekee cha taarifa za vituo na mwisho
utumiwe na wananchi kupata taarifa za huduma zinazotolewa na kituo
husika.
"Mpango
huu wa kielektroniki wa kuandaa mipango na kufanya maamuzi madhubuti wa
sekta ya afya nchini, tunaomba na tunahitaji sana kushirikiana katika
kuboresha huduma za afya na kuwatendea haki Watanzania," alisema.
Aliongeza
kuwa utatengeneza namba maalum kwa kila kituo kitakachoingizwa na namba
hiyo haitarudiwa hata kama kituo hicho kitafungwa.
Dk.Mmbando
aliwashukuru wadau mbalimbali kwa kushirikiana na Serikali kwa
kuhakikisha wanaleta maendeleo nchini na kuwaaagiza waganga kuhakikisha
wanafanya update kila wakati ili kuendana na wakati.
Kwa
upande wake Mkuu wa Kitengo cha Tehama Wizara ya Afya na Ustawi wa
Jamii, Hermes Rulagirwa alisema kupitia mfumo huo utatawawezesha kujua
sehemu ya kituo kilipo na huduma wanazozitoa.
Alisema kabla ya kuzinduliwa kwa mfumo huo wapo waganga kutoka vituo mbalimbali nchini walipatiwa mafunzo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269