.

DK. MAGUFULI NA RAIS KIKWETE IKULU BAADA YA KUIBUKA KIDEDEA URAIS KATIKA MATOKEO UCHAGUZI MKUU LEO

Oct 29, 2015

ma1
Rais Jakaya Kikwete akimpongeza kwa furaha, Ikulu jijini Dar es Salaam, aliyekuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, baada ya Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Mstaafu Damian Lubuva  kumtangaza Dk. Magufuli kuwa mshindi, alipotangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofayika Oktoba 25, mwaka huu.
mag2
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akimsomea sms za pongezi kutoka kila pembe ya dunia  mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM, Dk. John Magufuli, Ikulu jijini Dar es Salaam.
mag3
 Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli akipokea salamu za pongezi kutoka kwa aliyekuwa mgombea Urais kwa tiketi ya ACT Wazlendo, Mama Anna Mghwira, baada ya Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva kumtangaza kuwa mshindi, wakati akitangaza rasmi  matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako yeye na Rais Jakaya Mrisho Kikwete walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni. Dkt Magufuli amemshukur sana Mama Mghwira na kumwita mkomavu wa siasa na mwana-Demokrasia wa mfano jioni hii
mag4
mag5 mag6 mag7 mag8
Mama Salma Kikwete akimpongeza mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa Tais kutangaza matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni 
jioni hii
mag10
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongea kwa furaha mshindi wa kinyang’anyiro cha Urais kwa tiketi ya CCM na Rais Mteule Dkt John Pombe Joseph Magufuli mara baada ya Mwenyekiti wa  Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji Damian Lubuva  kutangaza rasmi matokeo ya uchaguzi mkuu Ikulu jijini Dar es salaam ambako walifuatilia kwa pamoja matangazo hayo ya moja kwa moja kupitia vituo vya televisheni jioni hii (Picha zote na IKULU)

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช