.

NAELEKEA KIJIJINI KWETU, NAWATAKIA NYOTE UCHAGUZI WA AMANI

Oct 25, 2015

Ndugu zangu,
Hii ni nchi yetu tuliyozaliwa. Ni nchi tunayoipenda sana. Tunashiriki leo, kama taifa moja, kulijenga daraja muhimu litakalounganisha
Jana na Kesho yetu. Hakuna mmoja wetu atakayeachwa nyuma, ni daraja tutakalovuka wote katika furaha na huzuni.
Kama taifa, Watanzania hatujawahi kushindwa mapambano yoyote tuliyoshiriki. Mara zote, siri kubwa ya ushindi wetu ni Umoja Wetu wa Kitaifa. Misingi ya mradi wa ujenzi wa Umoja wa Kitaifa iliwekwa na Mwalimu Nyerere na wenzake.
Uchaguzi huu usiwe chanzo cha kuibomoa misingi hiyo. Jana jioni nikiwa hapa Iringa nilifurahishwa sana kuwaona wafuasi wa Chadema na CCM wakitembea kwa pamoja wakitoka kwenye mikutano yao ya kufunga kampeni. Ni kielelezo cha Umoja wetu. Kielelezo cha Utanzania wetu wenye kutofautiana na wengine.
Ni imani yangu, ari na moyo huu, tutabaki nao hadi mwisho wa zoezi hili. Maana, kuna maisha ya kisiasa na kijamii, hata baada ya kukamilishwa kwa zoezi la uchaguzi.
Nikiwa njiani na makamanda wangu, kwenda kijijini kwetu kupiga kura, nawatakia nyote uchaguzi wa amani.
Maggid

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช