Rais wa Shirikisho la Mpira wa
Miguu nchini (TFF), Jamal Malinzi amewatumia salamu za pongezi wachezaji
Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu wanaochezea klabu ya TP Mazembe ya
Congo DR kufuatia kutwaa Ubingwa wa Ligi ya Mabingwa Afrika (CL) jana
kwa kuifunga timu ya USM Algiers kwa jumla ya mabao 4-1.
Katika salamu zake kwenda kwa
wachezaji hao, Malinzi amewapa hongera kwa mafanikio waliyofikia ya
kutwaa ubingwa huo wa vilabu Afrika, na kuwataka waongeze bidii ili
waweze kufanya vizuri pia katika michuano ya Kombe la Dunia la Mabara
litakalofanyika mwezi Disemba nchini Japan.
Malinzi amesema kwa niaba ya
familia ya mpira wa miguu na Watanzania wote wanawashukuru kwa
kuiwakilisha vizuri Tanzania kimataifa, na sasa moyo huyo wa kujituma
kwao waundeleleze katika mchezo dhidi ya Algeria wikiendi hii kuwania
kufuzu kwa fainali za kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269