Mbunge wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi
nahodha wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally 'Kaseja' nyaraka za
Pikipiki hiyo Dar es Salaam leo ambayo ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa
kikosi hicho wakati wa kampeni.(PICHA NA KHAMISI MUSSA)
Mbunge
wa Jimbo la Ilala Mussa Zungu (CCM) (mwenye kofia) akimkabidhi nahodha
wa timu ya Ferry Beach Boys, Selemani Ally 'Kaseja' namba ya Pikipiki
Dar es Salaam leo.
Zungu
amesema ilikuwa ni moja ya ahadi yake kwa kikosi hicho wakati wa
kampeni alipofika kituoni hapo wakati alipopita kumuombea kura aliyekuwa
mgombea Urais Mgufuli kupitia Chama cha Mapinduzi CCM ili iwasaidie
kujikusanyia kipato kwa njia hiyo ya kujikusanyia kipato ili wapate
nauli wanapokuwa wakienda kucheza kwenye pindi wapatapo mwaliko,
Mbunge huyo aliendelea kusema nitaendelea kusaidia maswala ya timu na
alipewa ombi la timu kusaidia vifaa vya michezo lakini leo nakusaidieni
Pikipiki iwe mali ya timu si mali ya mtu, anaendelea kusema Zungu,
alitowa ahadi ya Bodi ya Ferry na bodi hiyo ipo tayari tunasubiri
waraka uchapishwe na fikiri kabla ya mwezi wa kumi na mbili kwisha bodi
itakuwa imeundwa ili Soko hili liendeshwe na wafanya Biashara wenyewe,
na niliweka ahadi ya kuwawekea mahema kwenye maeneo ya wanaouza Samaki
maeneo ya wanaopigwa na Juwa na kabla ya mwezi wa kumi na mbili itakuwa
tayari.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269