Na K-Vis Media
SERIKALI ya awamu ya tano chini ya
uongozi wake Rais wa jamuhuri ya Mungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph
Magufuli imekunjua “makucha”, ambapo leo Ijumaa Novemba 27, 2015 Rais Dkt.
Magufuli amesimamisha kazi Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania, TRA Bw.Rished
Bade kufuatia ziara ya kushitukiza ya Waziri Mkuu Bw. Kassim Majaliwa mapema
leo asbhi pale Bandari ya Dar es Salaam.
Waziri Mkuu
Majaliwa, alibaini kupitishwa bila ya kulipiwa ushuru makontena 349 yenye
bidhaa na kusababisha hasara ya zaidi ya shilingi bilioni 80.
Kufuatia “Madudu hayo” Waziri Mkuu
aliagiza wale woooote waliohusika au wanaohusika na uhakiki na ruhusa ya
makontena hayo, wakamatwe mara moja.
Baada ya uamuzi huo, majira ya
Alasiri ya leo Ijumaa Novemba 27, 2015, Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe
Magufuli naye aliona hatua hiyo lazima iongezwe nguvu na kutangaza kumsimamisha
kazi mara moja Kamishna huyo Mkuu wa TRA.
na nafasi yake kukaimiwa na Katibu Mtendaji
wa Tume ya Mipango Dkt Philip Mpango.
Taarifa ya Katibu Mkuu Kiongozi
Balozi Ombeni Sefue, iliyotolewa na Ikulu ya Rais imesema, uteuzi huo unaanza
mara moja na wale woote waliotajwa kwenye kashfa hii ya sasa, hawataruhusiwa
kusafiri nje ya nchi hadi pale uchunguzi dhidi yao utakapokamilika.
Dkt. Philip Mpango, Kaimu Kamishna Mkuu wa TRA
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli
Hii ndiyo bandari ya Dar es Salaam,
ambayo kwa muda mwingi imekuwa ikihujumiwa na kutoa mapato yasiyolingana
na ukubwa na utendaji wake wake
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269