Afrika Kusini imesema kuwa, ina mpango wa kuondoa askari wake katika jimbo la Darfur la magharibi mwa Sudan.
Ofisi ya Rais Jacob Zuba wa Afrika Kusini imesema leo kuwa,
askari wa nchi hiyo wanaofanya kazi chini ya mwavuli wa kikosi cha
kulinda amani huko Darfur Sudan wataondolewa.
Ofisi hiyo imeongeza kuwa, askari wa jeshi la taifa la nchi hiyo
ambao wamekuweko Darfur tangu mwaka 2008 chini ya mwavuli wa kikosi cha
pamoja cha Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa, watarejea nyumbani
tarehe Mosi Aprili mwaka huu, tarehe ambayo ndipo zinapomalizika kazi
zao.
Hii ni katika hali ambavyo, hivi karibuni serikali ya Sudan
ilikanusha kuwa Umoja wa Afrika umeipa mwaliko rasmi wa kushiriki katika
mazungumzo ya amani na waasi.
Tangu mwaka 2003 serikali ya Sudan imekuwa ikipambana na makundi ya
waasi katika eneo la Darfur na kwenye mikoa ya Kordofan Kusini na Blue
Nile.
Kwa upande wake, ofisi ya kuratibu misaada ya kibinadamu ya Umoja wa
Mataifa imesema kuwa, hali ya kibinadamu huko Darfur ni mbaya sana na
kwamba kuna uwezekano watu 38 elfu wa Darfur Kaskazini wamekimbia makazi
yao.
Takwimu za Umoja wa Mataifa zinaonesha kuwa mgogoro wa Darfur
ulioanza mwaka 2003 umeshapelekea zaidi ya watu laki tatu kupoteza
maisha yao na milioni mbili na nusu kuwa wakimbizi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269