Breaking News

Your Ad Spot

Feb 18, 2016

TAFEYOCO WAMUOMBA MHESHIMIWA RAIS DKT. JOHN POMBE MAGUFULI AKUTANE NA VIJANA.

Na Anitha Jonas – MAELEZO.
Shirika lisilo la kiserikali la Tanzania Feminist and Youth Change Organization (TAFEYOCO) limemuomba Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuanzisha utaratibu wa kukutana na vijana ili kujadiliana mambo mbalimbali.
Hayo yamesemwa leo na Mwenyekiti wa Shirika hilo Bw. Elvis Makumbo alipokuwa akizungumza na waandishi habari jijini Dar es Salaam katika mkutano uliyolenga kumpongeza Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri aliyoifanya katika siku mia moja za uongozi wake.
“Vijana kwa sasa katika taifa ni wengi na ndiyo wenye uwezo wa kuleta maendeleo katika nchi na nguvu kazi ya Taifa na wanachangamoto nyingi hivyo Mheshimiwa Rais akijaribu kukutana nao nakuwasikiliza matatizo yao itasaidia kuleta mafanikio katika nchi na kujua nini kifanyike kuleta maendeleo katika Taifa,” alisema Bw. Makumbo.
Ameleza kuwa, Mheshimiwa Rais ameonyesha moyo wadhati wa kuwatumikia wananchi kwa kuwawajibisha watu wote walionekana wakitumia vibaya madaraka yao na kufanya ubadhirifu wa pesa za umma kinyume na taratibu za kiutumishi wa umma.
Mbali na hayo Bw.Makumbo amemuomba mheshimiwa Rais kufikiria kuanzisha mfumo au taasisi itakayohakiki mali za mtumishi wa umma na kuhoji ni namna gani mali hizo amezipata ili kupunguza wimbi la watumishi wa umma wanao tumia fedha za serikali vibaya kwa kujinufaisha wenyewe huku wakijiwekea utajiri mkubwa usiyolingana na kipato chao.
Mwenyekiti huyo aliendelea kumwomba Mheshimiwa Rais kuzidi kuzingozea nguvu taasisi za Serikali ili kuzijengea uwezo mkubwa wa kiutendaji mfano wa Taasisi hizo ni TAKUKURU na nyinginezo zinazosimamia mambo mbalimbali Yenye tija kwa Taifa.
Shirika hilo limesema Kauli Mbiu ya Mheshimiwa Rais ya Hapa Kazi Tu imeongeza hari kubwa ya utendaji kwa wananchi kwa kuwahimiza kuwajibika ikiwemo kwa watu wa sekta binafsi na taasisi za umma.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages