MWENYEKITI UWT MKOA WA DAR ES SALAAM AWANYOSHEA KIDOLE WALIOKISALITI CHAMA WAKATI WA UCHAGUZI MKUU
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth
Massaburi, akizungumza na wanawake wa umoja huo wa Wilaya ya Ilala Dar
es Salaam , katika mkutano wa kuwashukuru kwa kukipa ushindi Chama Cha
Mapinduzi (CCM) kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka
jana.
Mwenyekiti
wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth
Massaburi (kulia), akisisitiza jambo kwenye mkutano huo. Kutoka kushoto
ni Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Joel Kafuge, Mwenyekiti wa UWT Wilaya
ya Ilala, Apruna Humba na Katibu wa UWT Mkoa wa Dar es Salaam, Tatu
Maliaga.
Wanawake wa CCM Wilaya ya Ilala wakiwa kwenyev mkutano huo.
Mkutano ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
MWENYEKITI
wa Umoja wa Wanawake Tanzania wa Chama Cha Mapinduzi (UWT), Janeth
Masaburi amesema wanachama wa chama hicho waliokihujumu wakati wa uchaguzi mkuu uliofanyika mwishoni mwa mwaka jana wasitegemee kupata uongozi wowote ndani ya chama hicho.
Masaburi
alitoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanawake wa umoja huo wa Wilaya
ya Ilala Dar es Salaam katika mkutano wa kuwashukuru kwa kukichagua
chama hicho na kukipa ushindi ambapo kimeunda Serikali inayoongozwa na
Rais Dk. John Magufuli.
"Kunawenzetu
walitusaliti wakati wa uchaguzi mkuu na kuchangia mkoa wa Dar es Salaam
kushindwa kufanya vizuri hali iliyosababisha kuwepo na changamoto hata
ya kumpata Meya wenzetu hao tunawafahama na hawatapata nafasi ya kupata
nafasi ya uongozi ndani ya chama chetu" alisema Massaburi.
Massaburi
alisema ni heri kubakiwa na wanachama wachache waadilifu ndani ya chama
kuliko kuwa wengi ambao ni wasaliti na katika jambo hilo ataendelea
kulisimamia na kupigania maslahi ya chama ambacho anakitumikia.
Katika
hatua nyingine Massaburi aliwataka wana umoja huo kushikamana na
kushirikiana na kuhakikisha nguvu yao inaendelea kukipa ushindi chama
hicho wa kushika dola kwani jambo hilo linawezekana kwa asilimia 100.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269