WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA AFUNGUA DULA LA MSD WILAYANI CHATO
Mkurugenzi
Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD), Laurean Bwanakunu (kushoto), akitoa
maelezo kwa Waziri Mkuu Kassim Majaliwa kabla ya Waziri Mkuu hajafungua
duka la dawa la MSD Wilayani Chato juzi.
Waziri Mkuu Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto), akizungumza wakati akifungua dula la Bohari ya Dawa (MSD), Wilayani Chato.
Na Mwandishi Wetu
WAZIRI
Mkuu Kassim Majaliwa amefungua dula la Bohari ya Dawa (MSD), la
Wilayani Chato duka litakalotoa huduma kwa wananchi wa wilaya hiyo.
Akizungumza
katika hafla ya ufunguzi wa duka hilo Mkurugenzi Mkuu wa MSD Laurean
Bwanakunu alisema duka hilo ni mfano kwa Wilaya nyingine na mikoa,ambapo
tayari Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali Mitaa (Tamisemi) mikoa
na Wilaya kuanzisha maduka hayo,na kisha MSD itatoa ushauri wa
kitaalam.
Bwanakunu
alisema kwa kuanza,duka la dawa la Halmashauri ya Chato linaendeshwa na
MSD,lakini baada ya muda watalikabidhi kwa Halmashauri ya Chato.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269