Serikali ya Jamhuri ya Congo Brazzaville imeyataka mashirika mawili
makubwa ya simu nchini humo kukata mawasiliano yote wakati wa kufanyika
uchaguzi wa Rais hapo kesho.
Taarifa ya serikali ya Congo Brazzavile imeeleza kuwa, imeyataka
mashirika mawili makubwa ya simu ya MTN Congo na Airtel Congo kukata
mawasiliano yote ya simu hapo kesho wakati wa kufanyika zoezi la
uchaguzi wa Rais na vilevile siku ya Jumatatu. Kwa mujibu wa serikali
hatua hiyo imechukuliwa kwa sababu za kiusalama.
Waziri wa Mambo ya Ndani wa Congo Brazzavile ameziambia duru za
habari kwamba, uamuzi huo wa kutaka kukatwa mawasiliano ya simu
umechukuliwa kutokana na sababu za kiusalama.
Rais wa nchi hiyo Denis Sassou Nguesso anawania tena kiti hicho kwa
mara ya tatu na ametangaza kuwa ana matumaini makubwa ya kushinda licha
ya wapinzani wake kusema anaona ndoto za mchana. Wapinzani wa serikali
ya Brazaville wanasema kuwa, hatua ya kiongozi huyo ya kugombea kiti
hicho kwa mara ya tatu mfululizo inakiuka katiba ya Jamhuri ya Congo
Brazzaville.
Rais Nguesso ambaye ameingoza nchi hiyo kwa zaidi ya miaka 30, Oktoba
mwaka jana alibadilisha katiba na kuondoa kipengee kinachoweka ukomo wa
vipindi viwili kwa Rais na kujiandalia mazingira ya kubakia madarakani.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269