Mawaziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran na
Uturuki wamekutana na kufanya mazungumzo mjini Istanbul na kujadili
masuala ya uhusiano wa pande mbili, kieneo na kimataifa.
Dakta Muhammad Javad Zarif Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa
Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ambaye yuko nchini Uturuki kwa ziara rasmi
amefanya mkutano wa pamoja na waandishi wa habari akiwa na mwenyeji
wake, Mevlut Cavusoglu, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Uturuki. Dakta
Zarif amesema, misimamo ya Iran na Uturuki kuhusiana na matukio ya
Mashariki ya Kati inakaribiana sana na kwambva, Tehran na Ankara
zinasisitiza juu ya kulindwa umoja wa ardhi ya Syria.
Waziri Zarif amesema kuwa, Jamhuri ya Kiislamu ya Iran inapinga
baadhi ya njama za kutaka kuigawa ardhi ya Syria na kuongeza kuwa, siasa
za Tehran zimesimama juu ya msingi wa kuheshimu umoja na mamlaka ya
nchi zingine.
Aidha Waziri wa Mashauri ya Kigeni ya Iran amelaani shambulio la
kigaidi lililotokea leo katika mji wa Istanbul na kubainisha kwamba,
shambulio hilo lililo dhidi ya ubinadamu limezidi kuonesha sura mbaya ya
ugaidi.
Kwa upande wake Mevlut Cavusoglu, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa
Uturuki sambamba na kuashiria kwamba, Uturuki ina wakimbizi zaidi ya
milioni tatu kutoka Syria amesema kuwa, Tehran na Ankara zitafanya hima
ya kuhakikisha umoja wa ardhi ya Syria unahifadhiwa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269