Chama tawala nchini Afrika Kusini (ANC) kimesema kunapanga mikakati ya kumfikisha mahakamani kiongozi wa chama cha Economic Freedom Fighters, Julius Malema baada ya kusema kuwa atatumia silaha kukiondoa madarakani chama cha ANC.
Malema aliyasema hayo katika mahojiano yake na televisheni ya al Jazeera ya Qatar na kusisitiza kuwa, wako tayari kukiondoa madarakani chama tawala nchini Afrika Kusni kwa kutumia silaha na kwamba hata jeshi halitaweza kuwazuia.
Chama cha ANC kimetangaza kuwa kinavipa umuhimu vitisho hivyo na kwamba kitafungua mashtaka ya jinai dhidi ya Malema. Zizi Kodwa wa chama cha ANC amesema hilo si suala la haki za binadamu kwa mtu kutoa wito wa kumwaga damu.
Siku chache zilizopita chama cha upinzani nchini Afrika Kusini kilishindwa kupata kura za kutosha za kumsaiili na kumuondoa madarakani Rais Jacob Zuma kwa kutuhuma za kutumia vibaya mali ya umma.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269