Shirika la Afya Duniani (WHO) limetangaza kuwa, kuna uwezekano ugonjwa wa malaria utaangamizwa kabisa ifikapo mwaka 2020.
Ripoti iliyotolewa leo na WHO kwa mnasaba wa Siku ya Kimataifa ya Kupambana na Malaria imesema kuwa, kuna uwezekano kwamba ugonjwa huo utakomeshwa kabisa katika nchi sita za Afrika zinazosumbuliwa sana na malaria hadi kufikia mwaka 2020. Ripoti hiyo imeongeza kuwa, nchi hizo ni Algeria, Cape Varde, Swaziland, Bostwana, Afrika Kusini na Comoro.
Afrika Kusini imetangaza suala la kupambana na malaria kuwa ni lengo la kitaifa.
Takwimu zinaonesha kuwa, eneo la chini ya Sahara barani Afrika ndilo lenye idadi kubwa zaidi ya kesi za ugonjwa wa malaria unaosababishwa na mbu aina ya Anopheles. Asilia 88 ya wagonjwa wa malaria na asilimia 90 ya vifo vilivyosababishwa na ugonjwa huo katika mwaka uliopita wa 2015 iliripotiwa katika eneo hilo
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269