MKUU wa wilaya ya Kaskazini B Haji Makungu Mgongo akimkaribisha Naibu waziri wa afya Harusi Said Suleiman kuzindua wiki ya chanjo Afrika.
NAIBU Waziri wa Afya Harusi Said Suleiman akiwahutubia wananchi mbalimbali wliohudhuria katika sherehe hizo zilizofanyika kituo cha afya Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
KATIBU Tawala wilaya ya Kaskazini B Juma Abdalla Hamad akitoa maelezo namna wilaya ilivyojiandaa kufanikisha uzinduzi wa wiki ya chanjo Afrika katika sherehe ziliofanyika kituo cha afya Kitope.
Naibu Waziri wa afya akizindua Rasmi wiki ya chanjo Afrika kwa kumpatia tone la chanjo mtoto Mudrik Ali Khamis mkaazi wa Kitope Wilaya ya Kaskazini B Unguja.
Wananchi mbali mbali waliojitokeza katika kuitikia wito wa siku ya chanjo Afrika katika uzinduzi uliofanyika kituo cha afya Kitope.
KIKUNDI cha ngoma za asili cha Magereza kikitoa burudani katika sherehe za uzinduzi wa wiki ya chanjo Afrika.
Baadhi ya watoto waliojitokeza katika maadhimisho hayo wakisubiri huduma ya chanjo.
(PICHA NA ABDALLA OMAR HABARI MAELEZO ZA
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269