MBUNGE wa bunge la Afrika Mashariki, (EALA), kutoka nchini Burundi, Bi.Hafsa Mossi(pichani), ameuawa kwa kupigwa risasi na watu wasiojulikana maeneo ya Mutanga jijini Bujumbura.
Vyombovya Habari vinasema, Bi. Mossi aliyewahi kuwa Waziri na msemaji wa serikali ya Burundi mwanzoni mwa utawala wa Rais wa sasa Pierre Nkurunzinza, aliuawa baada ya kuteremka kwenye gari lake aina ya Mercedez Banz ili kulitazama baada ya kugongwa na gari lililowabeba wauaji wake.
Bi.Hafsa Mossi ambaye alikuwa mcheshi, aliwahi kuwa Mtangazaji wa Shirima laHabari la Uingereza BBC. Mauaji yake ni mtiririko wa matukio ya kuuawa kwa raia na watu mashuhuri nchini humo, mauaji ambayo wavhambuzi wa masuala ya kiusalama wanayaita "mauaji tata". Bi Mossi ameuawa siku moja tu tangu mazungumzo ya kutafuta ufumbuzi wa mzozo wa kisiasa nchini Burundi yaane mjini Arusha nchini Tanzania, chini ya upatanishi wa Rais mstaafu, Benjamin Mkapa. Hata hivyo mazungumzo hayo yalikwama, Jumatano Julai 12, baada ya Wawakilishi wa serikali kususa kuingia ukumbini, wakidai miongoni mwa washiriki walioalikwa na mpatanishi ndio wahusika wa jaribio la mapinduzi ya serikali ya Rais Nkurunzinza. Rais Nkurunzinza anapingwa na wanasiasa Wa upinzani baada ya kugonbea tena urais Wa nchi hiyo(muhula Wa tatu), kinyume na mkataba Wa Arusha.
Bi Mossi (kulia), enzi za uhai wake, akiwa na mbunge mwenzake kutoka Tanzania, Bi. Shy-Rose Bhanji
Wapita njia wakilitazama gari la Bi.Hafsa Mossi baada ya kuuawa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269