.

MCHENGERWA:HATUPASWI KUWA NA MIGOGORO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI

Jul 19, 2016

Mbunge wa Rufuji Mohamed Mchengerwa kulia,akisalimiana na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassani.


MBUNGE wa Rufiji Mohamed Mchengerwa ameiomba serikali kupeleka wawekezaji katika maeneo makubwa katika jimbo hilo ili kuwekeza ikiwa ni katika kukuza uchumi.


 Aidha amesema kiwanda cha sukari kitajengwa katika kata ya Mkongo katika kijiji cha Mbunju Mvuleni ambacho kuna hekta zaidi ya 40,000 na kiwanda hicho kinahitaji hekari 15000.


 Alisema rubada walitoa taarifa awali kuwa hakuna eneo Rufiji jambo ambalo si kweli kiwanda hicho kinahitaji heka 15,000 hivyo wanaweza kupeleka wawekezaji Zaidi ya watano.


“Tunataka mwekezaji aje wenyewe na sio kuwepo kwa madalali katikati na kwamba wananchi watashirikishwa katika kila hatua.


Tupambane tupate maeneo ili nilete wawekezaji ambao walitaka kujua kama ardhi ipo.

Hakikisheni hakuna ardhi inayotolewa inayotolewa bila wananchi kujua washirikishwe katika kila jambo. waziri wa kilimo kwamba ardhi tunayo hata wawekezaji zaidi ya watano wafike .Kijiji chetu tunaweza kupata hatimiliki nitashughulikia,”alisema.


Mchengerwa alishukuru wananchi na kuwaeleza ukweli kurejesha heshima ya rufiji katika taifa na kuahidi kusimamia masuala mbalimbali ikiwa ni pamoja na kuondoa tatizo la wafugaji na kujua maeneo ambayo kilimo kinategemewa na wafugaji hao.


 Akizungumzia hatua ya mifugo kuingia katika maeneo ya wakulima alisema kuwa wana idadi ya mifugo ambayo inapaswa kuwa katika eneo hilo na kwamba wapo watendaji wanaochukua rushwa na kuruhusu Ng’ombe kuingia katika maeneo hayo jambo ambalo ni kinyume kutokana na kuwa eneo hilo ni kubwa hivyo hakupaswi kuwa na migogoro kati ya pande hizo mbili.


 “Kwa kilomita hatupaswi kuwa na migogoro ya wakulima na wafugaji kutokana na ukubwa wa eneo. Nawaahidi katika kipindi changu cha miaka mitano migogoro ya wakulima na wafugaji itakwishwa kwani wanaochochea ni viongozi wasio waadilifu.Nataka niandike historia miaka yangu mitano nitafanya jambo nitajenga kiwanda cha sukari katika kata ya mkongo,”alisema.


 Afisa Maendeleo ya Jamii Joseph Magati,alisema Kampuni ya Africans dream imehadaa wananchi imekuwa ni migogoro ya wananchi na kampuni hiyo imeandika mikataba mikubwa lakini haitekelezi ilichoingilia mikataba.


 Alisema mashamba pori ndiyo sababu ya migogoro ya wakulima na wafugaji kwani maeneo mengi yameachwa tu hayalimwi na kwamba ng’ombe waliotakiwa kuwa katika eneo hilo ni 58,000 lakini kwa sasa wapo ngombe zaidi ya 200,000.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช