Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. Tulia Ackson akimuonesha Rais Dkt. John Pombe Magufuli sehemu ya
Madawati yaliyotengenezwa na fedha zilizopatikana kutokana na kubana matumizi
kutoka Ofisi ya Bunge katika viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akikagua Madawati hayo yaliyotengenezwa na Jeshi la Magereza
pamoja na Suma JKT
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akiwa amekaa kwenye moja ya Dawati katika hafla hiyo fupi ya ugawaji
wa Madawati hayo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akizungumza na Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya Msingi
Bunge George Samwel wakati akiangalia mfano wa darasa ya jinsi madawati hayo
yatakavyo katika katika shule mbalimbali nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akifurahia jambo na Wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge wakwanza kulia
Mariam Elias (darasa la tatu na wapili kutoka kushoto George Samwel mwanafunzi
wa darasa la tano wakiwa wanapiga makofi kabla ya tukio la ugawaji wa madawati
hayo yaliyotokana na kubana matumizi kutoka Ofisi ya Bunge.
Mwanafunzi wa darasa la tano katika shule ya Msingi
Bunge George Samwel akimtajia Mheshimiwa Rais Jina la Waziri Mkuu Kassim
Majaliwa mara baada ya kumuuliza huku Waziri Mkuu akitazama kwa furaha.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akimkabidhi Mbunge wa Ilala Mussa Azzan Zungu ambaye aliyapokea kwa
niaba ya Wabunge wa majimbo mbalimbali nchini.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Kamati ndogo ya Tume ya huduma za
Bunge inayoshughulika utengenezaji wa madawati. Waliosimama mbele ni Waziri
Mkuu Kassim Majaliwa, Mbunge wa Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa, Naibu
Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson, Mbunge wa Ilala Mussa Azan Zungu pamoja na
Waziri wa Ulinzi Dkt. Hussein Mwinyi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Wanafunzi wa Shule ya msingi
Bunge mara baada ya tukio la kukabidhi madawati katika Majimbo mbalimbali
nchini. Wengine katika picha ni Waziri Mkuu Kassim Majaliwa, Naibu Spika Dkt.
Tulia Ackson pamoja na Waziri wa Elimu Prof. Joyce Ndalichako
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akiwasalimia baadhi ya Maaskari brass bendi ya Jeshi la Magereza
mara baada ya kukabidhi Madawati
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe
Magufuli akiwasalimia baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Msingi Bunge katika
viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John
Pombe Magufuli akizungumza na Mwanafunzi wa Darasa la tatu katika Shule ya
Msingi Bunge Mariam Samwel wakati akiondoka kwenye viwanja hivyo
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli akisalimiana na Mbunge wa
Iringa Mjini Mchungaji Peter Msigwa aliyehudhuria hafla hiyo ya ugawaji wa
Madawati katika Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam. PICHA NA IKULU. HABARI KAMILI>>BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269