NA
K-VIS MEDIA/NA MASHIRIKA YA HABARI
KWA
uchache watu 80 wameuawa na wengine 18 wamejeruhiwa vibaya katika shambulio la
kigaidi mjini Nice Ufaransa usiku wa kuamkia Julai 15, 2016.
Taarifa
za vyombo vya habari zinasema, washambulizi walitumia lori, kuvamia umati wa
watu waliokuwa wakisherehekea Bastille Day kwenye mji wa Nice Kusini mwa
Ufaransa.
Gazeti
la Nice Matin lilimnukuu mwandishi wake aliyeko
eneo la tukio akisema, watu wengi wamejeruhiwa na damu imetapakaa kwenye mitaa.
Silaha
nyingi zilikutwa kwenye lori hilo na dereva wake ametambuliwa kuwa ni mkazi wa
mjini humo mwenye asili ya Tunisia.
Rais
wa Ufaransa Francois Holand, amesema shambulio hilo lina harufu ya ugaidi.
“Tuko
kwenye vita dhidi ya magaidi, wanaotaka kutuumiza kwa gharama yoyote.” Waziri
wa Mambo ya Ndani wa Ufaransa, Bernard Cazeneuve amesema.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269