Breaking News

Your Ad Spot

Sep 18, 2016

WAZIRI NAPE AZIDI KUWAHAMASISHA SERENGETI BOYS DHIDI YA CONGO BRAZAVILLE, AWAPA SH. MILIONI TANO ZA MOTISHA LEO

Waziri Nape akimkabidhi motisha ya sh. milioni 5,
Nahodha wa Serengeti Boys Issa Makame leo asubuhi
kuhamasisha timu hiyo ifanye vizuri
katika mechi yao dhidi ya Congo-Brazaville, leo
Na Shamimu Nyaki- WHUSM.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye, ametoa fedha taslimu sh. million 5, za motisha kwa timu ya Serengeti Boys, ili wachezaji wajitahidi kufanya vizuri katika mechi yao dhidi ya timu ya vijana wenzao ya Congo Brazivile, leo katika Uwanja wa Taifa Jjijini Dar es Salaam.

Waziri Nape amekabidhi fedha hizo leo asubuhi, Jijini Dar es Salaam, na kuwataka wachezaji hao kujituma zaidi katika mechi hiyo ili wapate ushindi utakaowawezesha kufuzu katika fainali za Mataifa ya Afrika kwa vijana  chini ya miaka 17 .

“Watanzania wote tupo  pamoja na nyie endeleeni kujituma kama mlivyofanya katika hatua ya kwanza na ya pili,  sisi Serikali tunawaunga mkono na tunawatakia kila la heri ili mlete heshima kwa Taifa.” Alisema Nape.

Waziri Nape ametoa fedha hizo, huku akiwa ameshatoa ahadi ya kutoa sh. 500,000/= kwa kila goli ambalo timu hiyo ya Serengeti Boys itafunga wakati wa mtanange huo wa leo.

Kocha wa timu hiyo  Bakari  Shime, amemhakikishia Waziri Nape na Watanzania kwa ujumla kuwa mechi ya leo watahakikisha wanapata ushindi kwani wamejiandaa vizuri na wachezaji wote wapo tayari kuivaa Congo Brazavile.

Pia Nahodha wa timu  Issa Abdi Makame, mbali na kuishukuru Serikali kwa motisha inayotoa ameahidi kujituma zaidi kwa kushirikiana na wenzake na kufuata maagizo kutoka bechi la ufundi  ili kuhakikisha wanapata ushindi.

“Tunashukuru sana kwa motisha mnayotupa na sisi hatutawaangusha tutajituma kadri ya uwezo wetu tupate ushindi  ili tusonge mbele zaidi ” Aliongeza Nahodha Makame.

Timu  hiyo ya vijana chini ya  umri wa Miaka kumi na saba (Serengeti Boys) inashiriki kufuzu kwa fainali za kombe la mataifa ya Afrika (AFCON) kwa vijana yatakayofanyika nchini Madagascar mwakani.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages