.

AFRIKA KUSINI YAANZISHA MCHAKATO WA KUJIONDOA ICC

Oct 21, 2016

media
Makao makuu ya ICC, Hague, Uholanzi.
Baadhi ya nchi za Afrika zimeanza kujiondoa katika uanachama wa Mahakam ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC). Siku nne baada ya rais wa Burundi kusaini sheria ya kuindoa nchi yake katika Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, Afrika Kusini imeanzisha mchakato wa kujiondoa kutoka uanachama wa mahakama hiyo.
Afrika kusini imechukua uamuzi wa kuanzisha mchakato huo kufuatia shinikizo ilikumbana nazo mwaka uliopita kutoka Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita za kuitaka imkamate rais wa Sudan Omar al Bashir wakati wa mkutano wa Umoja wa Afrika mjini Johannesburg.
Chini ya pigo la ombi la kusafirishwa, Rais wa Sudan Omar al-Bashir (katikati) amepiga picha ya pamoja na viongozi wa AU, Jumapili Juni 14.
Septemba mwaka jana, Mahakama Kuu ya Afrika Kusini iliinyima serikali ya nchi hiyo ruhusa ya kukata rufaa uamuzi ulioishutumu kwa kukosa kumkamata Omar al Bashir aliposhiriki mkutano huo mwezi Juni mwaka 2015.
Serikali ilijaribu kukata rufaa uamuzi wa Mahakama Kuu ikisema Bashir alikuwa na kinga ya urais kwa sababu yeye ni kiongozi wa taifa.
Lakini Jaji Hans Fabricius alisema rufaa hiyo haiwezi kufanikisha chochote.
“Afrika Kusini ni mwanachama wa Mkataba wa Roma uliounda Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita, na mkataba huo unabatilisha sheria zote ambazo huenda zingempa kinga Bashir asikamatwe na kushtakiwa”, amesema Jaji Hans Fabricius.
Kiongozi huyo wa Sudan amekuwa akisakwa na Mahakama ya kimataifa ya uhalifu wa kivita ICC kwa tuhuma za kutekeleza mauaji ya halaiki na makosa ya uhalifu wa kivita Darfur.
Omar ala Bashiri aliyechukua mamlaka kupitia mapinduzi ya kijeshi mwaka 1989 amekuwa akisakwa na Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu wa Kivita (ICC) kwa tuhuma za kutekeleza mauaji ya halaiki na makosa ya uhalifu wa kivita katika jimbo la Darfur, madai ambayo Bw Bashiri amekanusha.
Itafahamika kwamba nchi nyingi za Afrika zinailaumu ICC kwa kuzilenga zaidi nchi za Afrika.RFI

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช