Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amebadili hukumu zote za kifo nchini humo na kuzifanya kifungo cha maisha jela.
Hatua hiyo imewaondolea adhabu ya kifo wafungwa 2,747 katika
nchi hiyo ambayo haijamyonga mfungwa yeyote aliyehukumiwa kifo kwa
kipindi cha miongo mitatu sasa.
Taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Nairobi imesema, mbali na kupunguza
adhabu ya kifo cha wanaume 2655 na wanawake 92 na kuwa kifungo cha
maisha jela, Rais Uhuru Kenyatta pia amesaini hati ya msamaha na
kuachiwa huru mahabusu 102 waliokuwa wakihudumia vifungo vya muda mrefu.
Msamaha kama huo hutolewa kwa wafungwa wanaotambuliwa kuwa wamerekebika na kubadilika na wanastahiki kuachiwa huru mapema.
Kupunguzwa adhabu ya kifo kwa wafungwa wengi kulifanyika mara ya
mwisho nchini Kenya mwaka 2009 wakati wa utawala wa rais mtaafu Mwai
Kibaki.
Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema, hukumu ya kifo
ilitekelezwa mara ya mwisho nchini Kenya mwaka 1987. Hukumu hiyo
hutolewa kwa watu wanaopatikana na hatia za kutenda uhalifu kama ule wa
uhaini, mauaji na wizi wa kutumia nguvu.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269