NA
MAGRETH MAGOSSO,KIBONDO.
SHIRIKISHO
la Mpira Barani Ulaya (UEFA) kwa kushirikiana na Kampuni ya kutengeneza magari
ya Chivrolet ya Marekani imewakabidhi mipira 60 kwa ajili ya Soka la Watoto walio chini ya miaka 12 kwa shirika la
Umoja wa Mataifa UNHCR la kuhudumia wakimbizi katika Kambi ya Nduta iliyopo
wilaya ya Kibondo na Kakonko kwenye kambi ya Mtendeli zote za Mkoa wa Kigoma .
Akithibitisha
hilo juzi Mkuu wa UNHCR Kibondo Dost Yousafzai alisema wamepokea
mipira hiyo kwa nia ya kuwaunganisha na
kuthaminiana baina ya watanzania na warundi katika tasnia ya michezo hususani katika
soka la mpira wa miguu kwa watoto waishio kambini kwa kuwa wafrika wote ni
ndugu .
Alisema pamoja na UEFA na kampuni
hiyo kutoa kwa ajili ya kambi hizo,shirika la UNHCR wametoa mipira 20 kwa ajili
ya vijiji vinavyoishi karibu na kambi ya nduta ya kibondo na mipira 20 kwa vijiji
vinavyoishi jirani na kambi ya mtendeli,ili waratibu wa chama cha mpira
wilayani humo wagawe kwa timu hai ili kuimarisha michezo baina ya raia na
wakimbizi.
Akipokea mipira hiyo kwa niaba ya
wanakijiji Katibu wa Chama cha mpira
Kibondo James Evalist alisema kwa leo anachukua mipira 10 tu,na mipira miwili
aliikabidhi kwa timu ya Birutana ambayo inashiriki mashindano ya mechi za
ujirani mwema baina ya Burundi na Tanzania huku mipira 10 ikisalia kwa mkuu wa
UNHRC.
’ mipira ya watoto haihimili vishindo
kwa timu za wakubwa, siikatai na nawashirikisha wanamichezo wa kibondo lakini kama mmeamua kutusidia mlete mipira inayokidhi
mahitaji ya timu za wakubwa lakini tunaomba mturekebishie uwanja wa Mpira kwa
kuwa uwanja uliopo ni una kokoto tupu, alisema James.
Naye Kaimu Mkuu wa makazi Kambi ya
Nduta Jesca Ntaita alitoa mwito kwa Watanzania na Warundi wanaoishi katika makambi
ya wakimbi kufuata taratibu za nchi kwa kuwa kuna baadhi ya watanzania huingia
makambini kwa vibali vya warundi na warundi vivyo hivyo.
Na Mtendaji wa kijiji cha Biturana
Henry Thomas alisihi shirika la UNHCR kuwa waendeleze mashindano ya ujirani mwema
baina ya raia wa pande zote mbili waishio katika kambi hizo,kuwa yasiishie kambini
bali yaongeze wigo wa mashindano hayo.
Aidha kudhihirisha kuwa wanaweza
kusakata kabumbu timu ya kambi ya mtendeli iliwabugiza goli 4-0 dhidi ya Timu ya
kijiji cha Kasanda huku timu ya kambi ya
nduta iliwafunga bao 2 Timu ya Kijiji cha Biturana ya wilayani.mwisho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269