NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
IMEFAHAMIKA ,kuwa shughuli za kilimo,ufugaji holela,uchomaji
wa mkaa na uchimbaji wa madini ya Chokaa katika Hifadhi ya Msitu wa Makere
Kusini uliopo Halmashauri ya wilayani kasulu Mkoa wa Kigoma ni chanzo cha
mabadiliko ya tabia Nchi .
Shughuli hizo zimebainika kukithiri katika hifadhi hiyo,juzi baada
ya Kamati ya Ulinzi na Usalama Mkoa kwa kushirikiana na kamati ya wialani
humo,kutembelea hifadhi hiyo,ili kujionea uharibifu mkubwa uliofanywa na
wananchi kwa kushirikiana na wahamiaji haramu kutoka nchi jirani, kujikita
katika shughuli hizo,kinyume cha sheria
na taratibu za Nchi,ambapo hufanya hayo katika vyanzo vya maji na kitendo cha
kukata miti hovyo ni janga la ukame na mafuriko siku za usoni.
Meneja wa Misitu wilayani humo Donald Silaha alisema licha ya
uongozi wa wilaya kutoa agizo rasmi la wananchi waliovamia eneo hilo waondoke mara
moja lakini changamoto ya kutoka ni sugu kwa walengwa kwa kuwa wanadhani maisha
yapo katika msitu huo,bila kujali athari ya mabadiliko ya tabia nchi kwa leo na
kizazi kijacho.
Silaha alifafanua kuwa kushindwa kwa idara kuwajibika
kikamilifu inachangiwa na ukosefu wa vitendea kazi hasa gari la doria,mafuta na
uchache wa watumishi katika sekta hiyo nyeti ,kwa kuwa serikali imeajili watu
wachache na uhalisia wa jiografia ya wilaya ya kasulu ukiwemo msitu wa makere
ni tete kutokana na ukubwa wa msitu ,uharibifu uliofanywa ni mkubwa mno na
uvamizi ni mkubwa ilihali watumishi haba.
Akikaimu nyadhifa ya Mkuu wa wilaya ya Kasulu ,mkuu wa wilaya
ya Buhigwe Kanali Malko Gaguti alisema kila kukicha,wananchi hawataki kutoka
katika msitu wa makere kutokana na rutuba iliyopo,bila kupima athari ya uvamizi
katika msitu huo ambao unakatwa miti kila kukicha kwa ajili ya shughuli za
kilimo,uchimbaji chokaa huku wafugaji wakimaliza uoto wa asili kutokana na
mifugo kulishwa humo.
Mrakibu msaidizi idara
ya uhamiaji wilayani humo Emanuel Mpoyo aliongeza kwa kubainisha idadi ya
wahamiaji waliowakamata katika shughuli hizo ni 700,kitendo kinachochangiwa na
wananchi wa humo kushirikiana nao katika uvamizi wa hifadhi yam situ huo.
Akihitimisha hilo Mkuu wa Mkoa wa Kigoma Brigedia Mstaafu
Emanuel Maganga aliagiza kamati hizo zitumie kila njia kuhakikisha wanadhibiti
uvamizi holela wa wakulima,wafugaji
katika msitu huo ambao ni hazina kwa wilaya ya kasulu lakini wanaharibu
katikati yam situ huku nje msitu ukionekana mzuri ilihali ndani ni jangwa kwa
kuwa miti huvunwa kwa shughuli za uchomaji mkaa,kilimo,ufugaji na uchimbaji wa
madini.
Mwisho.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269