Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akipokea tiketi ya kusafiria muda mfupi kabla ya kusafiri kuelekea
Mwanza na abiria wa kawaida kwa ndege mpya ya Bombardier Q400 NextGen
kutoka kwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Prof. Makame
Mbalawa(kushoto) na Mkurugenzi wa Shirika la Ndege Tanzania Mhandisi
Ladisaus Matindi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akizungumza na waandishi wa habari muda mfupi kabla ya kupanda ndege
mpya za Bombardier Q400 NextGen kuelekea mkoani Mwanza kwenye ziara ya
kikazi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanya kazi wa ndege mpya za Bombardier
Q400 NextGen kuelekea mkoani Mwanza kwenye ziara ya kikazi.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan
akiwasalimu abiria waliosafiri nae kwenye ndege mpya ya Bombadier Q400
ya shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) akitokea Dar es Salaam kuelekea
jijini Mwanza kwa ziara ya kikazi.
Makamu wa
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewasili
jijini Mwanza ambapo kwa mara ya kwanza umetumia usafiri ya ndege ya
Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) aina ya bombardier Q400 kutoka Dar
es Salaam hadi Mwanza.
Makamu wa
Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza na waandishi wa habari katika
uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
kabla ya kusafiri na baada ya kuwasili mkoani Mwanza amewahimiza
wananchi kutumia usafiri wa ndege za ATCL kwa sababu ni wa bei nafuu na
usafiri wake ni wa uhakika.
Amesema
kwa kutumia ndege ya ACTL imemsaidia kupunguza gharama kubwa ya usafiri
kwa kutumia ndege za binafsi za kukodi kwa ajili ya safari za kikazi za
ndani ya nchi.
“Ni ndege zetu ni fahari yetu zipo Tanzania ni lazima sisi Watanzania tuzitumie ipasavyo kusafiria ndio maana na mimi leo nimeamua kutumia usafiri wa ATCL kwa sababu ni mzuri na wa uhakika”
Makamu wa
Rais amesema amefurahi kusafiri kwa mara ya kwanza na ndege hiyo kutoka
Dar es Salaam hadi Mwanza na amehimiza viongozi na wananchi kwa ujumla
kutumia usafiri wa ndege za ATCL ili kulipa nguvu shirika hilo katika
ufanyaji wake wa kazi kwa viwango bora zaidi.
Mara
baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege mkoani Mwanza, Makamu wa Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amepokelewa na
viongozi mbalimbali wa serikali na wa vyama vya siasa ambao waliongozwa
na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella.
Akiwa mkoani Mwanza, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan atafanya ziara ya kikazi siku NNE mkoani humo katika wilaya za Ukerewe,Ilemela,Nyamagana, Misungwi,Kwimba na Magu mkoani Mwanza. (P.T)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269