Katibu
Tawala wa Wilaya ya Temeke, Hashimu Komba (katikati), akikata utepe kwa
niaba ya mkuu wa wilaya hiyo, kuashiria kupokea madawati 80
yaliyotolewa na Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) kwa Shule ya
Msingi ya Kibasila Dar es Salaam jana. Wanaoshuhudia kutoka kulia ni
Msaidizi wa Mkuu wa wilaya hiyo, Betha Minga, Meneja wa TFS Wilaya ya
Temeke, Francis Kiondo na Mwakilishi wa Meneja wa TFS Kanda ya
Mashariki, Mohamed Lyandama
Ofisa Mistu wa Wilaya ya Temeke, Fredrick Umilla (kulia), akizungumza katika hafla hiyo ya kukabidhi madawati.
Meneja wa TFS Wilaya ya Temeke, Francis Kiondo (kulia), akitoa taarifa kwa mgeni rasmi.
Meneja
wa TFS Wilaya ya Temeke, Francis Kiondo (wa pili kulia), akimkabidhi
mgeni rasmi, Hashim Komba hati ya makabidhiano wa madawati hayo. Kutoka
kushoto ni Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Betha Minga na
Mwakilishi wa Meneja wa Kanda ya Mashariki wa TFS, Mohamed Lyandama.
Mgeni
rasmi Hashim Komba akipanda mti wa kumbukumbu mbele ya ofisi ya TFS
Wilaya ya Temeke iliyopo Chang'ombe Veta jijini Dar es Salaam.
Ofisa Elimu Vifaa na Takwimu wa Wilaya ya Temeke, Bakari Mrondwa akipanda mti.
Msaidizi wa Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Betha Minga
akishiriki kupanda mti.
Wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes wakishiriki kupanda mti. Kulia ni Masha Hassan na Yahaya Hamza.
Mgeni
rasmi akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wa TFS Wilaya ya Temeke
pamoja na wanafunzi wa Shule ya Msingi Wailes waliopokea madawati hayo
kwa niaba ya wenzao.
Na Dotto Mwaibale
WAFANYAKAZI
wa Wakala wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) Wilaya ya Temeke
wametakiwa kuendelea kuwa waadilifu katika kazi zao za kila siku ili
kujiepusha na vitendo vya rushwa kutoka kwa watu wanaojihusisha na
uharamia wa mali asili ya nchi.
Mwito
huo ulitolewa Dar es Salaam jana na Katibu Tawala wa Wilaya ya Temeke,
Hashim Komba kwa niaba ya mkuu wa wilaya hiyo wakati akipokea madawati
80 yenye thamani ya sh. 6,370, 000 yaliyotolewa na TFS wilaya ya Temeke
kwa ajili ya kukabiliana na uhaba wa madawati wilayani humo.
"Kwa
hali halisi ninayoiona hapa ofisini kwenu najua ninyi ni waadilifu
mnaviepuka vitendo vya rushwa endeleeni kusimamia kazi yenu ili kulinda
mali asili ya taifa" alisema Komba.
Komba
alisema kuwepo kwa magunia ya mkaa na mbao katika ofisi hiyo
zilizokamatwa na kielelezo tosha kuwa hakuna vitendo vya rushwa
vinavyofanywa na maofisa wa ofisi hiyo.
Komba amewaomba TFS kuendelea kuchangia madawati ili kumuunga mkono
Rais Dk. John Magufuli ya kuhakikisha wanafunzi wanasoma bure na katika mazingira bora ikiwemo kukaa kwenye madawati.
Akitoa
taarifa fupi wakati wa kukabidhi madawati hayo Meneja Wakala wa Huduma
za Misitu Wilaya Tanzania (TFS) Wilaya ya Temeke, Francis Kiondo alisema
wakala tangu kuanzishwa kwake wamepata mafanikio makubwa kupitia
utekelezaji wa mpango mkakati wa kwanza wa miaka mitatu 2011 -2014
ambapo sasa wanaelekeza nguvu katika kutekeleza mpango mkakati wa pili
wa miaka mitatu 2014 hadi 2016.
Alisema
katika kutekeleza majukumu yake wakala imepata changamoto za uvamizi wa
maeneo ya misitu kwa ajili ya kilimo, ufugaji, makazi, ukataji miti,
uchimbaji madini na uchomaji moto misitu.
Alisema
ili kukabiliana na changamoto hizo inatakiwa kuongeza watumishi na
vitendea kazi na kujenga vituo katika kila msitu wa hifadhi na kuweka
mabango ya tahadhari.
Kiondo
alisema kuwa wakala umetayarisha mpango bora wa usimamizi wa uhifadhi
wa misitu na moja ya mikakati iliyopo kwenye mpango huo ni kupanda hekta
185,000 za miti kwa mwaka kwa kushirikiana na wadau ili kuziba pengo la
mita za ujazo 19.5 milioni kwa mwaka za timbao hadi kufikia miaka 2030.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269