Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo, Augustin Matata Ponyo amesema leo kuwa amejiuzulu wadhifa huo
sambamba na mwafaka wa kisiasa uliofikiwa nchini humo ambao unamuongezea
muda wa kubakia madarakani Rais Joseph Kabila.
Kabila
alipasa kuondoka madarakani tarehe 19 mwezi Disemba. Hata hivyo
muungano unaotawala na baadhi ya makundi ya upinzani mwezi uliopita
yaliafikiana kuchelewesha uchaguzi wa rais hadi mwezi Aprili mwaka 2018
na kusisitiza kuwa, sababu kuu ya kuakhirishwa uchaguzi huo ni matatizo
ya kilojistiki katika kuwaandikisha wapiga kura na uhaba wa fedha.
Waziri
Mkuu aliyejiuzulu wadhifa huo wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya
Kongo ameviambia vyombo vya habari kuwa, amekabidhi hati ya kujiuzulu
kwa Rais sambamba na makubaliano ya kisiasa yaliyosainiwa tarehe 18
mwezi Oktoba mwaka huu.
Mrengo
mkuu wa upinzani nchini Kongo umepinga makubaliano hayo yalisainiwa
kati ya serikali ya Kinshasa na baadhi ya makundi ya kisiasa.
Itakumbukuwa kuwa watu zaidi ya 50 waliuawa mwezi Septemba mwaka huu
hmjini Kinshasa katika ghasia na maandamano ya mitaani ya wananchi
wakishinikiza kuondoka madarakani Rais Joseph Kabila.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269