.

UVCCM YAMGEUZIA KIBAO MBUNGE WA JIMBO LA SIMANJIRO JAMES OLE MILYA

Dec 1, 2016

James Millya
Na Woinde Shizza, Manyara
Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) umemjia juu Mbunge wa jimbo la  Simanjiro kwa tiketi ya Chadema, James Milya, na kusema kwamba malalamizko aliyotoa dhidi ya Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka Hamdu Shaka kudai alifanya mkutano wa hadhara hivi karibuni ni malalamiko ya kupika.

UVCCM imesema, malalamiko ya mbunge huyo niya uzushi kwa sababu kiongozi huyo Shaka Hamdu Shaka hakuwahi kufanya mikutano ya hadhara bali alizungumza na wanachama wa CCM  kwenye ofisi za chama cha Mapinduzi.


Pia Umoja  huo umesema anachoonekana kukilalamikia na kukihofia Milya ni kujaribu kwake kujikoasha mbele ya wananchi baada ya kuona kazi aliyoiomba ya kuwawakilisha  wananchi Simajiro ikionekana kumshinda  na kujikuta akijitisha kwa kivuli chake .

Msimamo huo umetolewa juzi  na Katibu wa UVCCM Wilaya ya Simajiro Bakari Mwacha alipoungumza na waandishibwa habari ofisini kwake mjini Simanjiro baada ya kimuona Mbunge wa jimbo hilo akilalamika katika baadhi ya vyombo vya habari akimsakama Shaka kwa madai aliyoyaita ni uongo na uzushi.

Mwacha alisema kiongozi yeyote wa chama cha siasa ana haki ya kukutana na  wanachama wake kwenye viakao vya ndani ili  kubadilishana mawazo, kupeana taarifa ilibkujua maendeleo na uhai wa chama na mwenendo wake bila kuzuiwa na sheria.

"Shaka alikutana na wanachama wa CCM  katika ofisi za UVCCM wilaya Simanjiro, akizindua jengo jipya la ofisi ya UVCCM kabla ya kufungua mashina ya wakereketwa katika kata za Naberere na Emboret , hakutubia mkutano wa hadhara, hatukuomba kibali polisi kwasababu ni mikutano ya ndani "alisema Mwacha.

Aidha Katibu huyo wa UVCCM alisema alichokifanya Shaka katika ziara yake ya siku mbili wilayani simanjiro  kinafanana na kinachofanywa na wajumbe wa kamati kuu ya Chadema akiwemo Waziri Mkuu Mstaafu Edward Lowassa na Feredrick Sumaye wanaozunguuka na kuzungumza na wanachamakwenye ofisi za Chadema.

Mwacha alisema hata Mwenyekiti wa CUF Profesa Ibrahim Lipumba naKatibu Mkuu wake  Maalim Seif Sharif Hamad ambao wako katika mvutano wa madaraka hukutana na wanachama wao hivyo si uchuro wala ajabu kwa Shaka kukutana na wanachama wa CCM mahali popote katika vikao vya ndani

Alisema Sumaye na Lowassa wanaongoza timu za makada wa chadema kufanya mikutano ya ndani wakikutana na wanachama wao kwenye ofisi zao kwa lengo la kujiimarisha kisiasa kama ambavyo Shaka na viongozi wenzake wanavyofanya katika mikoa mingiine.

Akifafanua zaidi, Mwacha alisema UVCCM katu hawawezi kukiuka agizo na amri ya Serikali kuhusu zuio la kutofanyika  mikutano ya hadhara wakati huu ambao wananchi wanatakiwa kufanya kazi za uzalishaji mali maeneo ya kazi, viwandani na mashambani.

"Milya anatafuta mtu wa kufa naye kisiasa baada ya kubaini amekwaa kisiki, siyo siri, wakati ukiwadia katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2020, ima fa ima atanyanyuliwa juu kwa juu na wananchi ikiwa hatawatumikia kama alivyowahidi mwaka 2015 " Alisisitiza Mwacha .

Mara baadavyabziaravyavShaka , Milya alionekana katika baadhi ya vyombo vya habari akimlalamikia kiongozi huyo kwa kuingia jimboni mwake na kufanya mikutano ya hadhara huku  akiwahamasisha wananchi na kutaka  Milya afungishwe virago ifikapo mwaka 2020  na wananchi .

Hata hivyo Katibu huyo wa UVCCM  wilaya Simanjiro alisisitiza kuwa viongozi wa UVCCM wataendelea na fatiki ya kufanya siasa na mikutano ya ndani yenye lengo la kukutana na wananchi bila kuhutubia  mikutano ya hadhara.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ª