.

BALOZI WA RUSSIA NCHINI UTURUKI AUAWA KWA RISASI

Dec 19, 2016

Balozi wa Russia nchini Uturuki amepigwa risasi na kuaga duani kwa majeraha baada ya kumiminiwa risasi wakati alipokuwa akihutubia kwenye maonyesho ya katika mji mkuu wa nchi hiyo Ankara.

Ripoti zinasema kuwa, balozi Andrey Karlov alishambuliwa kwa risasi katika eneo la sanaa ya uchoraji katika mji mkuu wa Ankara yaliyodhaminiwa na ubalozi wa Russia mjini humo.  Taarifa za awali zinasema kwamba, balozi huyo alikuwa akitoa hotuba wakati mtu aliyekuwa aliyekuwa na bunduki alipompiga risasi na kutoa ujumbe kwa lugha ya Kirusi.

Watu kadhaa wamejeruhiwa katika tukio hilo la kigaidi ambapo picha za tukio hilo zimewaonyesha watu wawili waliovalia nadhifu wakiwa wamelala chini ,karibu na kipaza sauti. Mshambuliaji huyo alisikika akitoa maneno kwa lugha ya Kirusi na kubandua baadhi ya picha zilizokuwa katika kuta za maonyesho hayo.


Balozi wa Russia nchini Uturuki akiwa chini baada ya kumiminiwa risasi
Maria Zakharova, msemaji wa Wizara ya Mashauri ya Kigeni wa Russia amethibitisha habari ya kufariki dunia balozi huyo.
Serikali ya Russia imelaani vikali shambulio hilo na kulitaja kuwa ni la kigaidi. 

Vyombo vya usalama vya Uturuki vimesema kuwa, mtekelezaji wa shambulio hilo alikuwa afisa polisi anayefanya kazi katika mji wa Ankara. Baadhi ya ripoti zinasema kuwa, maafisa wa polisi walifanikiwa kumpiga risasi mtekelezaji wa shambulio hilo na kumjeruhi vibaya huku baadhi ya ripoti zikisema ameuawa katika shambulio hilo la maafisa usalama.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช