.

BURUNDI YAKABIDHI TUHUMA ZA KUKIUKA HAKI ZA BINADAMU

Dec 18, 2016

Serikali ya Burundi imekana kwamba inakiuka haki za binadamu licha ya kuendelea mwenendo wa kutoweka raia nchini humo katika mazingira ya kutatanisha.
Hayo yamesisitizwa na maafisa wa serikali ya Burundi baaada ya jjumuiya mbalimbali za kutetea haki za binadamu hususan shirika la Iteka kutangaza kuwa, serikali ya Bujumbura inatumia siasa za kueneza woga na hofu baina ya wananchi na kwamba mwenendo wa kuuawa na kutoweka raia bado unaendelea.

Image Caption
Taasisi za kutetea haki za binadamu nchini Burundi zinasema kuwa, kumeripotiwa kesi nyingi za kutiwa nguvuni wapinzani wa serikali na baadaye kutoweka kabisa na kwamba watu wengine wanashindwa kutoka nje ya makazi na nyumba zao. 
Gaston Sindimwo, Makamu wa Kwanza wa Rais wa Burundi, amekanusha ripoti hiyo akisema kuwa, baadhi ya wapinzani wanaobeba silaha wanavuruga amani na nidhamu na kwamba watu kama hawa wanafikishwa mahakamani na kuchukuliwa hatua za kisheria.

0 Comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

ยช